Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, January 20, 2015

UKURASA WA 20; Geuza Changamoto Kuwa Fursa.

Changamoto au vikwazo unavyokutana navyo kwenye maisha vinaweza kukukatisha tamaa na vile vile vinaweza kuwa fursa nzuri ya wewe kufikia mafanikio.

Hakuna kitu chochote kinachotokea kwenye maisha yako ambaho huwezi kukigeuza kuwa fursa nzuri ya wewe kupata mafanikio zaidi.

SOMA; #HADITHI_FUNZO; Kikwazo Kinavyoweza Kugeuka Kuwa Fursa.

Katika kila tatizo unalipata, katika kila vikwazo unavyokutana navyo na katika kila changamoto unayopitia, hapo ndio kuna fursa kubwa ya wewe kubadili maisha yako.

Wakati unapitia matatizo/vikwazo/changamoto hizi angalia ni jinsi gani unaweza kunufaika nazo, usiishie tu kulalamika kwa nini matatizo hayo yaje kwako, bali kubali kwamba yameshatokea na angalia ni jinsi gani unaweza kunufaika na hayo yaliyotokea.

Ukiwa na akili ya kuwaza hivi utashangaa kuona mambo mengi yanawezekana na unaweza kufikia mafanikio uliyotarajia.

SOMA; Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba kwenye kila tatizo, vikwazo na changamoto ninazopitia kuna fursa kubwa sana kwangu ya kuboresha maisha yangu. Kuanzia sasa nitaacha kufikiria kwa nini tatizo hili lije kwangu tu na kuanz akufikiria ninawezaje kutumia tatizo hili kuboresha maisha yangu zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 21 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment