Moja ya vitu ambavyo vinawafanya wengi kuogopa kuchukua hatua ya kubadili maisha yao ni kuogopa kupotea. Yaani okuoghopa kushindwa au kuogopa hali kuwa mbaya kuliko ilivyo sasa hivi.
Ukweli ni kwamba ni heri upotee kuliko ubaki hapo ulipo. Maana utakapopotea utajifunza na kujua ipi ni njia sahihi. Ukibaki hapo ulipo utaendelea kujiaminisha kwamba siku moja mambo yatakuwa mazuri, kitu ambacho ni uongo mkubwa sana.
Kwa msisitizo zaidi ni heri kupoteza hela kidogo uliyonayo kuliko kubaki nayo na huku huifanyii chochote. Maana unapobaki nayo unajipa moyo kwamba una kahela kakukulinda na hivyo kuridhika. Ila unapoipoteza ni lazima akili yako itafanya kazi zaidi na utatafuta fedha zaidi.
Hivyo ndivyo maisha yalivyo, usiridhike na hapo ulipo, fanya kitu kifanye sasa.
JUST DO IT, hii ndio kauli mbiu ya mwaka 2015. Ifanyie kazi kila siku.
0 comments:
Post a Comment