Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, January 12, 2015

#HADITHI_FUNZO; Kijana Aliyenusurika Kuliwa Na Mamba.

Tajiri mmoja aliyekuwa anamiliki ardhi kubwa, wanyama na fedha nyingi alifanya sherehe ya kumwalika binti yake nyumbani. Binti huyu alikuwa amesafiri kwa muda mrefu nje ya nchi kimasomo. Kwenye sherehe hii tajiri huyu alialika watu wote katika aneo lile.

Sherehe ilikuwa kubwa na watu walikunywa na kufurahia, ilipofika usiku tajiri yule aliwaita vijana wote waliokuwepo kwenye sherehe ile na kuwaambia waende uwani kwake. Kufika uwani walikuta bwawa kubwa sana ambalo lilikuwa na mamba. Mamba wale walionekana kuwa na njaa na hasira kali sana.

Tajiri yule aliwaambia vijana wale kwamba atakayeweza kuingia kwenye bwawa lile na kuogelea na akaweza kutoka akiwa mzima atamka ekari elfu moja za mashamba yake. Na kama zawadi hiyo haitamtosha atampe fedha kiasi cha dola milioni moja na kama hiyo haitamtosha atamruhusu amuoe binti yake mrembo. Kabla hajamaliza kusema maneno yake akasikia kelele kwenye maji na ghafla kijana akatokea upande wa pili. Tajiri yule alimfata akishangilia akamwambia kijana wewe ni shujaa sana.

Tajiri yule akamuuliza je unataka nikupe shamba? Kijana akasema hapana. Akamuuliza tena je unataka nikupe dola milioni moja? Kijana akajibu hapana. Tajiri akasema, basi nafikiri unataka nikuoze binti yangu kijana akajibu hapana. Yule tajiri akapata hasira na kumuuliza kwa ukali; sasa wewe kijana ni kitu gani unataka? Kijana akamjibu, nataka kujua jina la yule aliyenusukuma kwenye hili bwawa….

Tunajifunza nini kwenye hadithi hii fupi?

Ili uweze kufanya mambo makubwa unahitaji kuhamasishwa. Kijana huyu kwa ridhaa yake asingethubutu kuingia kwenye maji yale ila kwa kuwa alishasukumwa na kuwa kwenye maji, lengo lake ilibidi liwe moja tu, kuondoka akiwa hai kwenye maji yale.

Ukiwa mwenyewe unaweza kuogopa kuchukua hatua, ila pale unapohamasishwa kufanya hivyo unaweza kujikaza na kupambana na hatimaye ukafika upande wa pili.

Tushirikishe na wewe umejifunza nini kwenye hadithi hii kwa kuweka maoni yako hapo chini…

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment