Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, January 19, 2015

UKURASA WA 19; Ishi Leo..

Leo ndio siku pekee unayoweza kuifurahia..

Leo ndio siku pekee unayoweza kuiathiri..

Leo ndio siku pekee unayoweza kuibadili..

Na leo ndio siku pekee unayoweza kuchukua hatua ya kuboresha maisha yako.

Cha kushangaza wengi hatuishi leo, tunapoteza muda wetu mzuri kwa kuishi jana na kuishi kesho.

Unaishi jana pale ambapo unaendelea kufikiria makosa uliyofanya na yakakuletea matatizo.

Unaishai kesho pale ambapo unakuwa na hofu kwamba kesho kitatokea nini.

Ukweli ni kwamba jana imeshapita, huwezi kuibadili kwa njia yoyote ile.

Kesho bado haijafika, na huenda usiione.

Kwa nini sasa usiishi leo, kufurahia wakati ulionao na kufanya maamuzi sahihi ambayo yataboresha maisha yako leo na hata kesho kama utakuwepo.

Jifunze kwa makosa uliyofanya jana na fanya maamuzi sahihi ambayo yataboresha maisha yako leo na hata kesho. Ila usipoteze muda wako kufikiria sana kuhusu jana au kuhofu sana kuhusu kesho.

TAMKO LA LEO;

Naamua kuishi leo, sitafikiria tena sana kuhusu jana, imeshapita nimechukua kile nilichojifunza. Sitahofu tena kuhusu kesho, bado haijafika hivyo kuhofu hakutasaidia. Nitafanya maamuzi sahihi leo, kwa wakati huu niliopo ambayo yataboresha maisha yangu ya leo na hata yajayo.

Tukutane kwenye ukurasa wa 20 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment