Usijenge nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi.
Inaonekana rahisi sana kusema hivyo, na hivi kweli unaweza kufanya hivyo?
Yaani mtu kakudoshishia uwanja wake, ufanyie shughuli zako kwa siku chache wewe ukaamua kujenga kabisa nyumba ya kudumu?
Kwa akili ya kawaida huwezi kufanya hivyo, kwa sababu unajua unakaribisha matatizo. Mwenye uwanja wake akiutaka nyumba yako inakuwa haina thamani tena. Na hata ukisema utaununua uwanja huo, wakati umeshajenga atakutajia bei anayotaka yeye kwa sababu anajua huna yena ujanja.
Sasa ni wapi ambapo unajenga nyumba kwenye uwanja wa kukodi?
1. Unapofanya biashara na mteja wako akawa mmoja, mteja huyu anaweza kuitikisa biashara muda wowote.
2. Unapoajiriwa na kutegemea ajira kwa maisha yako yote. Hata kama ajira itakusumbua hutaweza kuondoka maana maisha yako yanategemea hapo.
Usikubali kabisa kujenga nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi.
Unafanyaje sasa kama tayari umeshajenga nyumba kwenye uwanja wa kukodi?
Rahisi, nunua uwanja mwingine na anza kujenga nyumba yako.
Kama unafanya biashara inayokufunga anza kuipanua biashara hiyo.
Kama upo kwenye ajira unayoitegemea kwa asilimia 100 kwa kipato, anza kutengeneza vyanzo vingine vya kipato.
Bado hujui unawezaje kutanua biasara yako zaidi? Au hujui ni jinsi gani unaweza kutengeneza kipato cha ziada nje ya mshahara? Haya unaweza kujifunza kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Tembekea www.kisimachamaarifa.co.tz
Nakutakia kila la kheri.
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
0 comments:
Post a Comment