Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, January 19, 2015

#HADITHI_FUNZO; Kikwazo Kinavyoweza Kugeuka Kuwa Fursa.

Zamani kidogo mfalme mmoja aliagiza jiwe kubwa sana liwekwe kati kati ya barabara ambayo wanachi wake walikuwa wanapita. Kisha alikaa mahali na kuangalia kama kutakuwa na mwananchi atakayejaribu kuondoa jiwe lile.

Watu walipita, wakakuta jiwe lile, wengine walijipenyeza pembeni wakapita. Wengine walilalamika kwa sauti jinsi gani uongozi usivyojali kuweka bara bara katika hali ambayo zinapitika.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Baadae alipita mkulima mmoja aliyekuwa amebeba mazao yake anapeleka sokoni. Alipokutana na jiwe lile aliweka mzigo wake chini, na kujaribu kusukuma jiwe lile, ila kwa kuwa lilikuwa kubwa hakuweza kulisogeza. Alienda kichakani akarudi na mti mrefu alioutumia kama nyezo na akaweza kusogeza jiwe lile pembeni. Baada ya kuondoa jiwe lile aliona kifuko na alipokiokota alikuta sarafu nyingi za dhahabu kwenye kifuko kile. Pia alikuta kikaratasi kilichoandikwa na mfalme kwamba dhahabu ile ni zawadi kwa atakayeondoa jiwe lile.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

Unajifunza nini kwenye hadithi hii?

Kwenye kila changamoto unayokutana nayo hapo ndio kuna njia ya wewe kutokea. Acha kulalamika, acha kukwepa, bali chukua hatua ya kuikabili changamoto hiyo na utapata fursa kubwa sana ya kuboresha maisha yako.

Kumbuka kushiriki kwenye changamoto ya siku kumi ya kutokulalamika au kusemamabaya kwa wengine. Kwa maelezo zaidi soma; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Kila la kheri.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment