Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, January 14, 2015

Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

Kuna kauli nyingi ambazo watu wengi hupenda kutumia.
Katika kauli hizi kuna ambazo hutusukuma mbele na kutufanya tufikie malengo yetu.
Pia kuna kauli nyingine zinaashiria kushindwa na kukata tamaa. Kauli hizi zinaweza kukuzuia kufikia mafanikio makubwa.
Zifuatazo ni kauli mbili za kuacha kutumia leo ili kuweza kifikia malengo yako.
1. Liwalo na liwe.
Hii ni kauli ya kuashiria kutojali watu wengine na kujali maslahi yako tu. Kauli hii inaweza kukufanya uchukue hatua ambayo utaijutia sana baadae. Acha kutumia kauli hii na acha kufanya mambo yanayokunufaisha wewe tu na kuwaumiza wengine.
2. Kama ipo ipo tu.
Hii ni kauli inayoashiria kukata tamaa na hivyo kuacha kufanya juhudi ili kufikia malengo yako. Unaposema kama ipo ipo tu maana yake unakubali kwamba huwezi kutengeneza maisha yako. Maana yake unapokea chochote kinachokuja mbele yako. Kama unakubali chochote ni vigumu sana kufikia mafanikio.
Kumbuka kufikia mafanikio unahitaji malengo ambayo utayafanyia kazi kila siku. Usikate tamaa, endelea kuweka juhudi hata pale mambo uyanapoonekana kuwa magumu.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment