Hofu, hiki ni kikwazo cha watu wengi sana kufikia malengo yao na hata mafanikio makubwa.
Hofu ni matumizi mabaya ya ubunifu mkubwa ulioko ndani yako. Kila mtu anaubunifu na anaweza kutumia mawazo yake kutengeneza picha kubwa sana ya kuboresha maisha yake na ya wale ambao wanawazunguka. Kwa kutumia uwezo huu wa kuweza kuota na kufanyia kazi ndoto zako unaweza kubadili maisha yako kwa kiasi kikubwa.
Tatizo kubwa linalozuia wengi kuweza kutumia uwezo huo ni hofu. Watu huanzakufikiria vipi kama nikishindwa, vipi watu watanichukuliaje, je mambo yakienda vibaya itakuwaje. Kwa mawazo yote haya ni rahisi sana kuogopa kuanza na kushindwa kutimiza malengo yako.
Lakini ukweli ni kwamba haya yote unayofikiria hayapo, ni wewe tu unayatengeneza. Bado hujashindwa, ila unatengeneza picha ya kushindwa. Bado watu hawajakucheka, ila wewe umetengeneza picha ya watu kukucheka. Kwa hiyo yote yanayokukwamisha hayapo, umeyatengeneza mwenyewe.
Ukiweza kutumia vizuri nguvu yako hii ya uumbaji kutengeneza picha ya kuona kwamba umeshafanikiwa, watu wanafurahia kile unachofanya na umeweza kuvuka changamoto zako, itakusukuma sana kufikia malengo yako.
TAMKO LA LEO;
Kuanzia leo naamua kutumia ubunifu wangu kutengeneza mazingira mazuri ya kufikia ndoto yangu. Sitatumia ubunifu wangu kutengeneza mazingira ambayo yatanijaza hofu. Najua kwamba hofu ni kitu ambacho nakitengeneza mwenyewe. Naamua kuanzia leo kutotengeneza tena hofu ambazo zitanizuia kufikia mafanikio.
Tukutane kwenye ukurasa wa 18 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment