Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, January 22, 2015

UKURASA WA 22; Usiogope Kufanya Makosa…

Katika maisha, kazi na hata biashara kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho. Kitu hiko ni kwamba ni lazima utafanya makosa. Hata uwe umejiandaa kwa kiasi gani, hata uweke mambo vizuri kiasi gani bado utafanya makosa.

Hii ni kwa sababu hakuna mtu aliyezaliwa na kitabu cha matumizi kwamba maisha yako utayatumiaje. Ukinunua friji leo utapewa kitabu cha matumizi, ila unapopata mtoto haji na kitabu cha matumizi.

SOMA; USHAURI ADIMU; Unapokutana Na Tatizo Jiulize Jambo Hili Moja La Msingi.

Kuna kitu kizuri sana kuhusu makosa. Na kitu chenyewe ni kwamba makosa yanatufanya tujifunze zaidi ili kuwa bora zaidi. Bila makosa huwezi kujua ni njia ipi bora na ipi sio bora. Bila makosa huwezi kujua kama upo tayari au bado.

Makosa ndio njia nzuri ya wewe kujifunza, maana ukifanya makosa leo na ukaja ukarudia tena, mara ya pili inakuwa sio kosa bali umeamua.

Hivyo usiogope kufanya makosa, bali penda kujifunza kupitia makosa yako ili usiyarudie tena.

TAMKO LA LEO;

Najua makosa ni sehemu ya maisha yangu. Sitaogopa kufanya makosa maana nisipofanya makosa sitajifunza kitu chochote. Nitatumia makosa yangu kama sehemu ya kujifunza. Sitarudia tena kosa ambalo nimeshalifanya kwenye maisha yangu, kwa sababu mara ya pili litakuwa sio kosa tena bali ni uamuzi wangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 23 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Sheria NANE Za Kufanikiwa Kwenye Biashara Kutoka Kwa Warren Buffett.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment