Kulikuwa na kundi la watu ambao walikuwa wamesimama kando kando ya mto. Mara watu wale walisikia sauti ya mtoto akilia kwenye maji. Walistuka sana kuona mtoto analia na kuzama kwenye maji. Mtu mmoja kwenye kundi lile aliruka haraka na kwenda kumwokoa mtu yule.
Wakati akiwa kwenye maji, mara wakasikia sauti ya mtoto mwingine akilia kwenye maji, mtu mwingine tena akaruka kuingia kwenye maji kumuokoa mtoto yule. Wakasikia tena mwingine na mwingine na mwingine, watu wote wakawa wameshaingia kwenye maji na wanahangaika kuokoa watoto wale.
SOMA; Kauli KUMI Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Nelson Mandela.
Akawa amebaki mtu mmoja ambaye hakuingia kwenye maji na akawa anaanza kuondoka. Wenzake walimuuliza kwa hasira unaenda wapi badala ya kuokoa watoto? Akawajibu nafuata mto huu kujua ni nani anayetupa hawa watoto kwenye maji.
Tunajifunza nini hapa?
Kuna mengi ya kujifunza; kwanza badala ya kukimbilia tu kutatua tatizo unaloliona ni vyema kujua chanzo cha tatizo ni nini. Maana unawez akung’ang’ania kutatua tatizo na ndio yakaongezeka.
Pia unapoona mtu hajihusishi na tatizo kwa wakati usikimbilie kumlaumu, anaweza kuwa anatafuta nini chanzo cha tatizo.
Tushirikishe ulichojifunza kweye hadithi hii kwa kuweka maoni hapo chini.
SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.
0 comments:
Post a Comment