Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, January 9, 2015

UKURASA WA 09; MUDA–Kitu Chenye Thamani Kubwa Ila Kisichothaminika Na Wengi.

Muda ni kitu chenye thamani kubwa sana kwenye maisha yako. Poteza fedha hata iwe nyingi kiasi gani, unaweza kuitafuta tena. Ila ukishapoteza muda ndio imetoka, huwezi kuutengeneza tena hata kama ungekuwa na fedha kiasi gani.

Kitu kingine muhimu ni kwamba muda ndio kitu ambacho binadamu wote tumepewa kwa usawa. Watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa wote wana masaa 24 kwa siku, hakuna anayeweza kuongeza zaidi ya hapo.

Tofauti kati ya waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa ni matumizi ya muda wao. Waliofanikiwa wanatumia muda wao vizuri kufanya mambo yanayowazalishia zaidi. Wasiofanikiwa hujiona wana muda mwingi sana na hivyo kuupoteza kwa kufanya mambo ambayo hayana uzalishaji kwao.

Ili uweze kubadili maisha yako na kufanikiwa sana mwaka huu 2015 ni lazima uweke vipaumbele kwenye matumizi ya muda wako. Hakikisha kila muda unaotumia unautumia kwa manufaa ya maisha yako, ikiwemo muda ambao unapumzika.

Jambo kubwa na la kushangaza ni wale ambao wana matumizi mazuri ya muda wao hujiona hawana muda wa kuwatosha ila wakipewa majukumu ya ziada huweza kuyapatia muda wa kuyafanya. Wale ambao hawana matumizi mazuri ya muda wao hujiona wana muda mwingi sana ila wakipewa jukumu la kufanya hawapati muda wa kulikamilisha.

TAMKO LA LEO.

Natambua kwamba muda ni kitu chenye thamani sana. Pia natambua kwamba muda ukishapotea haurudi tena. Kuanzia leo nitatumia muda wangu vizuri kufanya mambo ambayo yana faida kwangu na yatakayoniwezesha kuboresha maisha yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa kumi kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment