Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, January 29, 2015

UKURASA WA 29; Kitu Pekee Unachoweza Kuwa Na Uhakika Nacho…

Kitu pekee unachoweza kuwa na uhakika nacho ni kutokuwa na uhakika.

Hujanielewa? Tumia mifano hii;

Unapanga kwamba utakwenda kwenye mkutano, umeambiwa mkutano utaanza saa sita na kumalizika saa nane. Wewe unapanga baada ya mkutano wa saa nane, saa nane na nusu utakutana na mtu muhimu sana. Unapanga mambo yako vizuri kabisa na unakuwa na uhakika utamaliza mkutano wako saa nane na saa nane na nusu utakutana na mtu muhimu.

Unakuja kupata changamoto pale ambapo mkutano uliotakiwa kuisha saa nane unaendelea mpaka saa nane na nusu na hauna dalili z akumalizika. Huku mtu muhimu uliyepanga kuonana naye akikutafuta kwamba tayari amefika na anakusubiri. Mkutano huwezi kuondoka kabla haujaisha na mtu muhimu anakusubiri. Unafanya nini?

Hapa ndipo mtu unaanza kupata msongo wa mawazo, kukasirika, na hatimaye kukosa vyote viwili.

Hakuna mtu ambaye ana uhakika na jambo lolote. Unapanga utawahi mahali kwa mwendo wa nusu saa, unafika njiani unakutana na ajali na magari hayawezi kupita. Unapanga utawahi ndege kwamuda uliopangwa ili uweze kuwahi kitu muhimu, dakika za mwisho unaambiwa safari imeahirishwa.

Hakuna mwenye uhakika, na hili pekee ndio tuna uhakika nalo.

SOMA; Sababu TATU Kwa Nini Watu Wengi Wanashinda Kufikia Mafanikio.

Unafanya nini sasa? Je unakubali kila kitu kiende hovyo kwa sababu huna uhakika?

Hapana, huwezi kuacha kila kitu kiende hovyo kwa sababu huna uhakika. Badala yake unahitaji kujiandaa mapema kabla ya kitu. Na pia jipe nafasi ya kuweza kurekebisha chochote kitakachokea katikati.

Kwenye mfano wa mkutano hapo juu, unaweza kutenga saa moja ya ziada ili usipange ratiba ambazo zitaingiliana.

TAMKO LA LEO;

Kitu pekee ambacho nina uhakika nacho ni kutokuwa na uhakika. Kuna mambo mengi sana yatakayotokea saa moja ijayo ambayo sikutarajia kama yangetokea. Kila mara nitajiandaa mapema ili kuepuka mambo yangu kuvurugika kutokana na kutokuwa na uhakika.

Tukutane kwenye ukurasa wa 30 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Hiki Ndio Kitakachotokea Miaka 100 Ijayo..

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment