Huwa tuna utaratibu wa kupunguza ukali wa maneno, kwa kiswahili tunaita tafsida.
Yaani badala ya kusema mtu amezaa tunasema amejifungua, japokuwa yote ni yale yale tu, ila kujifungua linapunguza ukali wa uhalisia wenyewe.
Maneno kama kujisaidia, kufanya tendo la ndoa na mengine mengi ni maneno mazuri yanayotumika badala ya maneno halisi ya vitendo hivi. Uzuri wa maneno haya ni kwamba yanapotumika kila mtu anajua maana ni ile ambayo unafichwa.
SOMA; Ushauri Kwa Wajasiriamali Kutoka Kwa Mwanzilishi Wa Facebook.
Sasa kuna neno moja ambalo lina tafsida yake, ila watu huwa wahaielewi kabisa hii tafsida. Neno hilo ni KAWAIDA.
KAWAIDA ni neno ambalo linatumika kuficha ukweli halisi ambao ni HOVYO.
Ukisema unafanya kazi kawaida maana yake unafanya HOVYO, kwa kiwango cha chini sana ambacho hakuna anayeweza kuvutiwa.
Ukisema wewe ni mfanya biashara wa kawaida maana yake wewe ni mfanyabiashara wa HOVYO ambae hujui unakoelekea na unafuata tu upepo.
SOMA; NENO LA LEO; Kuhusu Kinachokurudisha Nyuma.
Usikubali kabisa kuwa wa kawaida, namaanisha kuwa hovyo.
Chochote unachofanya, kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana ili yeyote atakayeona avutiwe, ashawishike kujua zaidi na hapa ndio thamani yako inaongezeka. Hata kama unafanya kazi ambayo unaona haiwezi kufanywa kwa kipekee wewe ibadili na ifanye kwa kiwango cha hali ya juu sana. Utaona mabadiliko makubw akwenye kazi yako na hata maisha yako kwa ujumla.
Ukikubwali kuwa wa kawaida, yaani kuwa HOVYO, umeamua kutopata mafanikio ambayo yanakusubiri. kuwa bora, kuwa tofauti, kuwa wa kipekee na utaona mafanikio yakikufuata wenyewe.
Kuanzia leo jiwekee marufuku kuwa HOVYO.
0 comments:
Post a Comment