Ukweli ni kwamba, pale unapoanguka au kushindwa watu wanafurahia sana.
Unaweza kuona sio kweli lakini ndio hali halisi ilivyo.
Watu wengi wanaokuzunguka wanaweza kufurahia sana pale unapofanikiwa. Lakini pia unapoanguka kuna watu wanaofurahia sana.
Hawafurahii kwa sababu wanakuchukia wewe ila maisha yao ndio yanawalazimisha kufurahia hali hiyo.
Watu wengi wana maisha magumu sana, hivyo wakiona kuna mtu mwingine ana maisha magumu zaidi yao wanapata ahueni, kwamba angalau na wao hawako wenyewe.
Hii inawafanya wafurahi na hii inatokea kisaikolojia bila hata ya kulazimisha.
Hujawahi kuona mtu anamweleza mwenzake mataizo halafu wanaanza kushindana ni nani mwenye matatizo mengi?
Unamwambia mtu mimi nina matatizo kweli, sina fedha, nina mgonjwa, na kazi/biashara haziendi vizuri. Yeye anakwambia hunifikii mimi, sina hela kabisa, watoto wanahitaji ada na kazi sina.
Ukweli ni kwamba kila mmoja kati yenu anakuwa anafurahia kwamba sio yeye tu ana matatizo.
Unapoingia kwenye matatizo, jitahidi uweze kuyatatua na usonge mbele, wengi wa watakaokuwa wanakupa moyo wanafurahia wewe kuwepo kwenye matatizo hayo.
0 comments:
Post a Comment