Siku moja ng'e alikuwa upande mmoja wa mto na alitaka kuvuka na kwenda upande wa pili akapate chakula. Ila nge hawezi kuogelea kwenyue maji. Wakati amekaa pale akitafakari achukue hatua gani akamuona chura.
Ng'e alimfata chura akamwambia chura wewe unaweza kuogelea kwenye maji, tagadhali nisaidie nifike ng'ambo ya pili nikapate chakula.
Chura alimwambia siwezi kufanya hivyo, wewe ni ng'e na ng'e wanauma na wanasumu kali, utaniuma nife.
Ng'e akamsihi chura, akamwambia nakuahidi sitakuuma, ninahitaji kweli kufika upande wa pili.
Chura akaona huruma na kukubali ombi lile. Alimwambia ng'e apande mgongoni kwake na safari ya kuvuka mto ikaanza. Wakiwa katikati ya mto mara ng'e akamuuma chura. Chura akamuuliza ng'e kwa hasira, mbona umeniuma? Ona sasa tutakufa wote.
Ng'e akamjibu, mimi ni ng'e na ng'e huwa wanauma...
UNAJIFUNZA NINI KWENYE HADITHI HII?
Kuna watu unawaonea huruma kwenye maisha yako ila watu hao ndio wanaokurudisha nyuma.
Watu hawa wanaweza kuwa hawajui kama wanakurudisha nyuma ila ndio maisha yao yalivyo.
Wajue watu hawa kwenye maisha yako na waepuke. La sivyo mtaendelea kuzama pamoja.
0 comments:
Post a Comment