Akija mtu na kukuambia kuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio, kimbia haraka sana na usiendelee kusikiliza. Maana ukiendelea kusikiliza unaweza kujikuta umeshaanza kushawishika.
Hakuna nia ya mkato ya kufikia mafanikio, na kama ipo mafanikio utakayoyapata hayatadumu.
SOMA; Sheria 12 Kwa Wanaoanza Biashara Kutoka Kwa Bilionea Mark Cuban.
Kila kitu kinahitaji muda wa kukua ndio kiweze kufikia mafanikio. ukilazimisha kitu kabla ya muda wake utatengeneza madhara makubwa sana.
Kama jinsi ilivyo kwamba huwezi kuwapa wanawake tisa mimba moja ili waibebe kwenye mwezi mmoja, ni lazima mimba ikae miezi tisa ndio aweze kuzaliwa mtoto mwenye afya njema na atakayeweza kumudu maisha ya kawaida. Hivyo ndivyo ilivyo kwenye kufikia mafanikio. Vitu vyote vizuri kwenye maisha vinahitaji muda.
Usikate tamaa pale unapoona unafanya kila kitu lakini bado huoni mafanikio. Jua kwamba muda muafaka bado, endelea kuweka juhudi. Muda muafaka utakapofika utashangaa kuona mafanikio yanatokea kila kona mpaka utajiuliza yalikuwa yamejificha wapi.
SOMA; Maswali Matatu Kwa Anayetaka Kuwa Mjasiriamali Kujiuliza Kutoka Kwa Richard Branson.
Unapoweka malengo na mipango yako, hakikisha unakomaa nayo na acha kuangalia vishawishi vya pembeni. Hivi vitakuchelewesha wewe kufikia malengo yako. Badala ya kupoteza muda wako kutafuta njia ya mkato, tumia muda huo kuimarisha njia yako ya kufikia mafanikio.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio. Kila kitu kizuri kwenye maisha kinahitaji muda ili kuweza kukifikia. Nitaendelea na malengo na mipango yangu hata pale nitapokuwa sioni mabadiliko. Najua siku muafaka ikifika mafanikio yatakuja kama mvua. Na nitakuwa tayari kuyapokea.
Tukutane kwenye ukurasa wa 26 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment