Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, January 13, 2015

UKURASA WA 13; Jifunze Kila siku.

Hitaji la chini kabisa la wewe kufikia mafanikio kwenye eneo lolote kwenye maisha yako ni kujifunza kila siku. Ni muhimu sana wewe kujifunza kila siku, jifunze kuhusiana na kazi au biashara unayofanya, jifunze kuhusiana na maendeleo binafsi, jifunze kuhusu fedha na uwekezaji na jifunze kuhusu maisha kwa ujumla.

Dunia ya sasa inabadilika kwa kasi sana, vitu ambavyo vilikuwa vinamaana miaka kumi iliyopita, leo havina maana tena.

Biashara au kazi ambayo inalipa leo, miaka kumi au ishirini inaweza isiwepo kabisa. Ni muhimu sana wewe kuwa mbele ya wengine kwa kujua nini kinaendelea na kuziona fursa mapema kabisa.

Utaweza yote haya kama utakuwa na utaratibu mzuri wa kujifunza.

Unajifunzaje sasa?

Kwanza kama unafuatilia KURASA 365 ZA MWAKA 2015 tayari ni sehemu ya kwanza ya wewe kujifunza, kwa sababu kila siku unapata kitu kipya cha kuulisha ubongo wako na kinachokuchokoza ufikiri zaidi.

Pia unaweza kujifunza kwa kusoma vitabu, hii ni lazima kama kweli upo makini na kufikia mafanikio. Kama hujawahi kabisa kusoma kitabu anza sasa kwa kujiwekea lengo la kusoma kitabu kimoja kwa mwezi, baada ya hapo weka lengo la kusoma kitabu kimoja kwa wiki, halafu ongeza zaidi kwa kusoma vitabu viwili kwa wiki. Kadiri unavyozidi kuongeza muda wa kusoma, ndivyo unavyoongeza maarifa na kuongeza kipato chako.

Pia unaweza kujifunza kwa kuhudhuria semina mbalimbali zinazoendeshwa au hata kujisajili kwenye kozi mbalimbali zinazotolewa. Uzuri ni kwamba sio lazima ukae darasani ndio usome, siku hizi unaweza kujifunza mambo mengi kupitia mtandao.

Soma; Kozi 1100 unazoweza kujifunza bure kupitia mtandao.

Hili ni hitaji la msingi kwako, JIFUNZE KILA SIKU.

TAMKO LA LEO;

Najua kwamba kujifunza kila siku ni hitaji muhimu sana ili niweze kufanikiwa. Kila siku nitatenga angalau saa moja ya kujisomea na kujifunza mambo mapya. Nitatafuta maarifa yatakayoniwezesha kuziona na kuzityumia fursa zinazonizunguka.

Tukutane kwenye ukurasa wa kumi na nne hapo kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment