Bwana mmoja alikuwa na mke wake ambaye walipendana sana. Ilitokea yule mwanamke akawa anaumwa sana na asingeweza kupona. Wakati anakaribia kukata roho alimwambia mume wake nakupenda sana, tafadhali niahidi kwamba hata kama nikifa hutampenda mwanamke mwingine. Na kama ukivunja ahadi hiyo mzimu wangu utakujia na utakutesa sana.
SOMA; Sehemu Tano Unazoweza Kupata Mtaji Wa Kuanzia Biashara.
Mume wake alikubaliana nae na akaweka ahadi hiyo. Muda ulipita baada ya mwanamke yule kufa na mwanaume yule aliepuka kuwa na mwanamke mwingine. Baadae ilitokea akakutana na mwanamke ambaye walipendana sana na waliamua kuoana. Wakati wanakaribia kufungua ndoa mzimu wa mwanamke yule ulianza kumtokea yule mwanaume kila siku usiku. Mzimu ule ulimlalamikia kwa kutokutunza ahadi na kila siku usiku ulikuwa ukimtokea na kumwambia kila kitu ambacho mwanaume yule aliongea na mke wake mtarajiwa siku hiyo.
Hali hii ilimchosha yule mwanaume na akaamua kuomba ushauri kutoka kwa mzee mwenye busara. Mzee yule alimwambia inaonekana mzimu huu una akili sana. Mwanaume yule alimjibu ndio, maana unaweza kuniambia kila kitu kinachoendelea. yule mzee alimwambia nitakupa dawa moja ambayo utaitumia mzimu huo ukija.
SOMA; NENO LA LEO; Kuhusu Kufikia MAFANIKIO MAKUBWA.
Usiku uliofuata mzimu ule ulikuja tena, yule mwanaume aliuambia, wewe ni mzimu ambao una akili sana, na unajua siwezi kukuficha chochote, kama utaweza kunijibu swali hili moja, nitaahirisha ndoa yangu na sitaoa tena. Mzimu ukamjibu uliza swali lako. Yule bwana aliingiza mkono wake kwenye mfuko na kuchukua maharage na kufungua mkono, kisha akauuliza mzimu ule, niambie ni maharage mangapi yako kwenye mkono wangu. Kwanzia pale mzimu ule ulipotea na haukurudi tena.
Tunajifunza nini kwenye hadithi hii?
Mzimu ni kitu ambacho tunajitengenezea kwenye akili zetu, hauwezi kujua kitu ambacho hatukijui. Kama unafikiria wewe umelogwa, umechezewa, una kisirani, ni wa kushindwa hayo yote umejenga mwenyewe kwenye kichwa chako. Ondokana na mawazo hayo na utaweza kufanya chochote unachotaka kwenye maisha yako.
Nakutakia kila la kheri.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
SOMA; Mambo Matano(5) Ambayo Ni Marufuku Kufanya Kwenye Eneo La Kazi.
Da hapo vipi tena?
ReplyDelete