Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, January 18, 2015

UKURASA WA 18; Hakuna Anayejali Maisha Yako Zaidi Yako Mwenyewe.

Kuna wakati ambapo tunajali sana kuhusu watu wengine wanavyojali kuhusu maisha yetu.

Tunafikiri kwamba watu wengine wanatufuatailia kila tunachofanya na hivyo kuhofia watatuchukuliaje hasa kama tutashindwa.

SOMA; Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku.

Ukweli ni kwamba hakuna anayejali maisha yako zaidi yako mwenyewe. Hakuna ambaye anakosa usingizi akifikiria wewe unafanya nini. Hata kama atakuona ukifanya na kukupinga au kukukatisha tamaa, dakika chache baadae atakuwa maeshasahau.

Hakuna anajali maisha yako zaidi yako wewe kwa sababu kila mtu ametingwa na maisha yake. Kila mtu anafikiria matatizo na changamoto anazokutana nazo kwenye maisha yake na hivyo hana muda mwingi wa kukufuatilia wewe kama unavyofikiri.

SOMA; Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

Fanya kile ambacho unaona ni sahihi kwako. Usiangalie au kufikiria wengine wanasemaje au watakufikiriaje, wao wenyewe wametingwa na maisha yao.

TAMKO LA LEO;

Najua maisha yangu ndio kipaumbele changu. Hakuna mtu mwingine anayeyajali maisha yangu zaidi yangu mwenyewe. Kila mtu ametingwa na maisha yake. Nitafanya kile kilicho sahihi bila ya kujali wengine watasema nini au watanifikiriaje. Maana mwishowe mimi ndiye nitakayeendelea na maisha yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 19 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment