Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, January 5, 2015

#HADITHI_FUNZO; Chochote Kinachotokea Huwezi Kujua Ni Kizuri Au Kibaya

Palikuwa na mkulima mmoja ambaye alikuwa anamiliki farasi wake waliyekuwa anamsaidia shughuli mbalimbali.
Siku moja farasi yule alitoweka na hakuonekana tena. Wanakijiji wenzake walikuja kumfariji na kumpa pole kwa pigo alilopata.
Yeye aliwauliza nani ajuaye kama kilichotokea ni kibaya au kizuri?
Watu wale waliondoka huku wakimshangaa.
Siku chache baadae farasi yule alirudi na farasi wengine kumi.
Wanakijiji wenzake walikuja kumpongeza kwa farasi wale wengi.
Aliwaambia tena nani ajuaye kama kilichotokea ni kibaya au kizuri?
Waliondoka huku wakishangaa.
Siku chache baadae mtoto wa kiume wa mkulima yule alidondoshwa na mmoja wa farasi wale wapya na akavunjika mguu.
Wanakijiji wale walimtembelea tena kumpa pole kwa kijana wake kuumia.
Mkulima yule aliwauliza tena, nani ajuaye kama kilichotokea ni kibaya au kizuri?
Watu wale waliondoka kwa hasira.
Siku chache baadae ilitoka amri ya vijana wote wenye afya kukusanywa na kujiunga na jeshi ili kwenda kupigana vita, kijana wake akaachwa.
Watu wale wakaja tena...
TUNAJIFUNZA NINI HAPA?
Chochote kinachotokea kwenye maisha unaweza kukichukulia ni kibaya au kizuri.
Chochote unachokiona kibaya kina faida kubwa ndani yake, kazi ni kwako kuitafuta.
Kila la kheri.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment