Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, January 6, 2015

NENO LA LEO; Kitu Hiki Kimoja Kitakufanya Uache Kukosoa Wengine

Let the refining and improving of your own life keep you so busy that you have little time to criticize others. –H. Jackson Brown, Jr.

Fanya jukumu la kubadili na kuboresha maisha yako liwe muhimu sana kwako na lichukue muda wako mwingi kiasi kwamba ukose muda wa kukosoa wengine.

Binadamu tunapenda sana kukosoa wengine ili hali sisi wenyewe mambo yetu sio mazuri.

Ni rahisi sana kumnyooshea mtu kidole na kusema yule kafanya hiki, mara kasema hivi na wakati huo huo maisha yetu yanatuhitaji sana ili tuweze kuyaboresha.

Weka kipaumbele kwenye kuboresha maisha yako, kufani kafanya nini, fulani kasema nini hayo hayakuhusu. Wazungu wanasema it is none of your business.

Nakutakia siku njema.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment