Mabadiliko yoyote unayotaka kufanya kwa mwaka huu 2015 anzia hapo ulipo na anza na ulicho nacho.
Usijidanganye unasubiri mambo yawe mazuri, ukweli ni kwamba hayatakuwa mazuri, kila siku ina changamoto zake.
Kama umepanga kuanza biashara anza sasa, anza na kile ulicho nacho. Kama huna cha kuanza kabisa, fikiria kitu ambacho unaweza kufanya, ambacho kuna watu wako tayari kukulipa kwa kukifanya, anza kukifanya, waoneshe watu, kiboreshe zaidi ili kiwasaidie wengi zaidi na endelea kukua kuanzia hapo.
Kama unataka kupata uzoefu wa kitu fulani, omba hata kufanya kazi kwa kujitolea ili kujifunza hiko unachotaka.
Kama hutaanza sasa kwa kutumia ulicho nacho uwezekano mkubwa ni kwamba hutaanza kabisa na mwaka huu utapita kama miaka mingine ilivyopita.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni JUST DO IT, KAMA KUNA CHOCHOTE UNACHOFIKIRIA KUFANYA ANZA KUKIFANYA. Mengine utajifunza na kurekebisha mbele ya safari.
TAMKO LA LEO.
Naanzia hapa nilipo, naanza na hiki nilichonacho(vitaje), sitapoteza tena muda kwa kufikiri kuna wakati utakuwa sahihi. Wakati sahihi ni sasa na ninaanza kuleta mabadiliko kwenye maisha yangu.
Tukutane kwenye ukurasa wa sita kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
0 comments:
Post a Comment