Mafanikio yana upendeleo mmoja, yanaenda kwa watu ambao wanafanya mambo kwa ubora wa hali ya juu sana.
Hawa ni watu wameamua kwenda hatua ya ziada kwenye jambo lolote wanalofanya. Hawakubali tu kufanya kama kila mtu anavyofanya. Watu hawa wanajua unapokwenda hatua ya ziada unajijengea nafasi kubwa ya kufikia mafanikio makubwa.
SOMA; Kuwa Kawaida Ni Kupoteza Muda Wako Na Siri Moja Ya Mafanikio Mwaka 2015
Fanya zaidi ya unavyolipwa, kama umeajiriwa timiza majukumu yako na nenda hatua ya ziada. Fanya mambo mazuri na bora ambayo wengine hawafanyi.
Kama upo kwenye biashara, fanya zaidi ya mteja anavyotegemea. Nenda mbali zaidi, mshangaze mteja na aone huduma aliyoipata hawezi kuipata sehemu nyingine yoyote. Kwa hali hii utatengeneza wateja wengi sana.
Mafanikio yote yapo kwenye hatua ya ziada. Kama ilivyo kwenye kupanda ngazi au mlima. Chini kunakuwa na watu wengi na hivyo kunakuwa na kelele nyingi. Ila unavyozidi kwenda juu unakuta watu wachache na hewa ni nzuri sana.
SOMA; KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba ili kufikia mafanikio nahitaji kwenda hatua ya ziada, nahitaji kufanya tofauti na wengine wanavyofanya na kufanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Kazi yoyote nitakayoifanya, biashara yoyote nitakayoifanya na hata maisha yangu kwa ujumla nitafanya kwa ubora wa hali ya juu na kwa upekee. Nitafanya zaidi ya ninavyotegemewa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 31 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment