Watu wengi wanafikiri kwamba kama wakiwa na watu wanaowapenda basi watakuwa na furaha kwenye maisha yao.
Watu wengi wanafikiri kwamba wakiwa na fedha nyingi ndio watakuwa na furaha.
Watu wengi wanafikiri kwamba wakishaondokana na changamoto za maisha ndio watakuwa na furaha.
Watu wengi wanafikiri kwamba kama maisha yasingekuwa magumu wangekuwa na furaha.
Yote haya ni uongo, hakuna kitu chochote au mtu yeyote anayeweza kukuletea furaha ila wewe binafsi.
Hata uwe na watu ambao wanakupenda kiasi gani kama huna furaha hawawezi kukupatia furaha.
Kama sasa hivi huna fedha na huna furaha, ukiwa nazo fedha nyingi ndio utazidi kukosa furaha zaidi.
Kama unasubiri maisha yasiwe magumu ndio uwe na furaha, nasikitika kukuambia kwamba utakufa bila ya kuwa na furaha.
Furaha inaanzia ndani kwako na inaanza na wewe mwenyewe hapo ulipo na kwa ulichonacho.
Una kila sababu ya kufurahia maisha yako hata kama ni magumu kiasi gani. Anza kuhesabu vile vizuri ulivyonavyo sasa na utaweza kufurahia maisha yako.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba furaha hailetwi na mtu, kitu au hali. Furaha inatoka ndani yangu mwenyewe. Kuanzia leo naamua kuyafurahia maisha yangu. Nafurahi kwa sababu mpaka sasa nipo hai, nina afya njema, naweza kusoma hapa na pia naweza kubadili maisha yangu. Kwa kuwa nina furaha ninao uhakika wa kufikia mafanikio makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa kumi na tatu kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
0 comments:
Post a Comment