Monday, April 27, 2015
Sunday, April 26, 2015
NENO LA LEO; Tulichozaliwa Nacho Na Tulichojifunza….
Love is what we were born with. Fear is what we learned here. -Marianne Williamson
Upendo ndio kitu ambacho tulizaliwa nacho. Hofu ni kitu ambacho tumejifunza hapa duniani.
Upendo utakuletea furaha kwenye maisha, upendo utakuwezesha kufanya kile unachopenda na kufanikiwa na upendo utakuwezesha kuishi na wengine vizuri.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyodhulumu Maisha Yako Wewe Mwenyewe.
Hofu ndio sumu kubwa ya mafanikio. Hofu itakuzuia wewe kuchukua hatua, hofu itakufanya ujione wewe huwezi, hustahili. Na hofu zote hizi umejifunza hapa duniani.
Usikubali hofu ziendelee kukurudisha nyuma.
Nakutakia siku njema.
Saturday, April 25, 2015
NENO LA LEO; Ufunguo Mkuu Wa Furaha.
Love is the master key that opens the gates of happiness. -Oliver Wendell Holmes
Upendo ndio ufunguo mkuu unaofungua milango yote ya furaha.
Umesoma vizuri hapo juu, upendo ndio ufunguo wa furaha, sio fedha nyingi, sio umiliki wa mali za kifahari na sio kutoka kwa mtu.
Kama unataka kuw ana furaha kwenye maisha yako, kuwa na upendo. Wapende wote wanaokuzunguka na kubali kupendwa na wengine pia.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Kitu Hiki Kimoja Ni Muhimu Kuliko Kiwango Cha Fedha Unachotaka.
Friday, April 24, 2015
NENO LA LEO; Hakuna Uhaba Wa Fursa, Kuna Uhaba Wa Kitu Hiki…
There is no scarcity of opportunity to make a living at what you love; there's only scarcity of resolve to make it happen. -Wayne Dyer
Hakuna uhaba wa fursa za kutengeneza kipato kwenye kile unachopenda; kuna uhaba wa wewe kuamua kufanya hivyo.
SOMA; Njia Ya Uhakika Ya Kufikia Mafanikio Makubwa.
Kitu chochote ambacho unapenda kufanya, kuna fursa nyingi sana za kuwez akutengeneza kipato. Kama unapenda kupika keki, unaweza kutengeneza keki kwa ajili ya kuuza, unawez akuandika kitabu chenye maelezo ya jinsi ya kutengeneza keki nzuri, unaweza kurekodi video ukionesha hatua kwa hatua utengenezaji wa keki na mengine mengi ambayo mtu mwingine atakuwa tayari kulipia.
Lakini yote hayo yatatokea kama wewe utaamua yawe hivyo. Kama utakaa chini na kufikiri na kufungua macho yako ili uweze kuziona fursa mbalimbali zinazokuzunguka.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Sababu Namba Moja Kwa Nini Hufanikiwi Kwenye Kazi Unayofanya.
KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.
AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.
Wednesday, April 22, 2015
NENO LA LEO; Najua Umeshasikia Hili Mara Nyingi, Sio Vibaya Ukasikia Tena Na Leo.
I know you've heard it a thousand times before. But it's true - hard work pays off. If you want to be good, you have to practice, practice, practice. If you don't love something, then don't do it. -Ray Bradbury
Najua umeshasikia hili mara elfu moja kabla. Lakini ni kweli- kufanya kazi kwa juhudi kunalipa. Kama unataka kuwa vizuri, unahitaji KUFANYA, KUFANYA, KUFANYA. Kama kuna kitu ambacho hukipendi, usikifanye.
SOMA; Kazi Ndio Msingi Wa Maendeleo.
Hakuna mbadala wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Nafikiri huwa nasema hili karibu kila siku. Ndio moja ya misingi ambayo naisimamia kwenye maisha yangu. Misingi mingine ni UAMINIFU, UADILIFU na NIDHAMU.
Umeajiriwa, tekeleza majukumu yako kwa ufanisi wa hali ya juu sana. Weka juhudi zako zote na ubunifu wako kuifanya kazi yako kuw aya kipekee, usiangalie ni kiasi gani unalipwa, toa kile ulichonacho wewe kwanza na kama aliyekuajiri hataona thamani yako, wengine wataiona.
Umejiajiri au unafanyabiashara, thamani unayozalisha ndio itakufanya uendelee kuwa na kipato. Weka juhudi na maarifa kwenye kile unachofanya, hakikisha wanatumia bidhaa au huduma zako wananufaika sana.
Kuna kitu ambacho hupendi? Achana nacho, usikifanye, usikifuatilie. Tuna ishi kwneye dunia yenye uhuru mkubwa, hakuna anayekulazimisha chochote, halafu muda ni mfupi sana, mpaka uanze kufuatilia kila kitu.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Njia Mbili Za Kukuondolea Matatizo Yako Ya Kifedha.
KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.
AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.
Tuesday, April 21, 2015
NENO LA LEO; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuishi Maisha Yako Kwa Ukamilifu.
Work like you don't need the money. Love like you've never been hurt. Dance like nobody's watching. -Satchel Paige
Fanya kazi kama vile huhitaji fedha. Penda kama vile hujawahi kuumizwa. Cheza kama vile hakuna anayekuangalia.
Ukiweza kufanya mambo hayo matatu, utaishi maisha yako na mafanikio yatakuwa yako.
SOMA; Hii Ndio Sababu Kwa Nini Watu Wanafurahia Pale Unapoanguka...
Unapofanya kazi kama vile huhitaji fedha, utaweka nguvu zako zote na ubunifu wako mkubwa. Kwa hali hii utafanya kazi iliyo bora sana na utafikia mafanikio makubwa.
Unapopenda kama vile hujawahi kuumizwa unatoa upendo wako wote na bila ya kuangalia ni nini umewahi kupitia. Ukianza kuleta hisia zako za kuumizwa utaharibu tena mapenzi mapya.
Unapocheza kama vile hakuna anayekuangalia, unacheza vile unavyotaka wewe, bila aibu, bila kufikiria wengine wanakuchukuliaje. Na hivi ndivyo unavyotakiwa kuyaishi maisha yako. Bila kujali sana wengine wanasemaje kuhusu wewe.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.
Monday, April 20, 2015
NENO LA LEO; Kama Hutaki Kuwa Na Maadui Fanya Kitu Hiki Kimoja.
He who falls in love with himself will have no rivals. -Benjamin Franklin
Yule anayejipenda mwenyewe hawezi kuwa na maadui/wapinzani.
SOMA; Siri Za Kuwa Mjasiriamali Bora Na Kufikia Mafanikio Makubwa.
Njia moja ya uhakika ya kuepuka kuwa na maadui ni kujipenda wewe mwenyewe. Unapojipenda wewe mwenyewe utawapenda na wengine pia. Na mtu yeyote anayewapenda wengine bila ya ubaguzi ni vigumu sana kuwa na maadui.
Na hata pale watu watakapolazimisha kuw ana uadui na wewe, hilo halitakuwa tatizo kwa ko kwa sababu hutakuwa na muda wa kufuatilia hayo.
Jipende wewe mwenyewe, utawapenda wengine pia na utaondokana na maadui zako.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wanaotafuta Ajira. Soma Hapa Uone Fursa Unazoweza Kutumia.
Sunday, April 19, 2015
NENO LA LEO; Hii Ndio Sifa Muhimu Ya Mtu Unayetakiwa Kumuajiri.
Do not hire a man who does your work for money, but him who does it for love of it. -Henry David Thoreau
Usimuajiri mtu anayefanya kazi yako kwa sababu tu anataka fedha, bali ajiri yule anayeifanya kwa sababu anaipenda.
Fedha sio hamasa nzuri ya kufanya kazi. Hii ni kwa sababu hakuna kiwango cha fedha ambacho mtu anaweza kuridhika nacho. Na mtu anapofanya kazi kwa ajili ya fedha tu, hakuna kitu kingine anachojali.
Ila mtu anayefanya kazi wka sababu anaipenda, ataweka juhudi na maarifa, atakuwa mbunifu na hii itamwezesha kufanya kazi yake kwa ubora wa hali ya juu sana. Katika hali hii atakufanyia kazi bora na yeye atapata kipato kizuri.
Nakutakia siku njema.
SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.
Saturday, April 18, 2015
NENO LA LEO; Njia Ya Uhakika Ya Kufikia Mafanikio Makubwa.
If you want to be successful, it's just this simple. Know what you are doing. Love what you are doing. And believe in what you are doing. -Will Rogers
Kama unataka kufikia mafanikio, ni rahisi kama hivi. Jua ni nini unafanya. Penda kile unachofanya. Na pia amini kile unachofanya.
SOMA; Siri Za Kuwa Mjasiriamali Bora Na Kufikia Mafanikio Makubwa.
Jua kile unachofanya, kama hujui ni vigumu sana kufikia mafanikio. Jua ni nini unafanya na unataka kikufikishe wapi.
Penda kile unachofanya. Unapopenda unachofanya inakufanya wewe kuwa na hamasa kubwa na kuweka juhudi na maarifa hata pale unaposhindwa.
Amini kile unachofanya, mafanikio yanaanza na imani yako. Je unamini unachofanya kitakufikisha wkenye mafanikio, je unaamini kinawanufaisha wengine.
Vitu hivyo vitatu vitakufikisha kwenye mafanikio bila ya kujali ni kitu gani unafanya kwenye maisha yako.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Sababu Zinazokufanya Wewe Kushindwa Kuthubutu Wazo Lako
Friday, April 17, 2015
NENO LA LEO; Unachotakiwa Kusema Na Unachotakiwa Kufanya.
I say what I want to say and do what I want to do. There's no in between. People will either love you for it or hate you for it. –Eminem
Nasema kile ninachotaka kusema na nafanya kile ninachotaka kufanya. Hakuna kuwa kati kati(vugu vugu). Watu watakupenda au kukuchukia kw akile unachosema na kufanya.
SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wanaotafuta Ajira. Soma Hapa Uone Fursa Unazoweza Kutumia.
Usiseme kitu kwa sababu unataka kuwafurahisha watu. Usifanye kitu kwa ajili ya kuwafurahisha watu. Unaweza kuwafurahisha wachache ila pia utawachukiza wengine.
Kama watu watakuchukia kwa jambo ambalo hata wewe hulipendi, maisha yako yanaweza kuwa magumu zaidi.
Ni bora ufanye kile unachotaka kufanya, sema kile unachotaka kusema. Kuna ambao watakupenda kwa hilo na watakupa moyo wa kufanya zaidi. Na kuna ambao watakuchukuia na kukupinga kwa hilo, hawa hawatakusumbua kwa sababu kile ulichosema au kufanya ndio unachopenda au kujali.
Kitu kinapokuwa na maana kwako na kama sio kinyume na sheria na taratibu basi usihofu kuhusu wachache watakaokupinga.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Siri Za Kuwa Mjasiriamali Bora Na Kufikia Mafanikio Makubwa.
Thursday, April 16, 2015
NENO LA LEO; Usilenge Mafanikio. Lenga Kitu Hiki Na Mafanikio Yatakuja Yenyewe.
Don't aim for success if you want it; just do what you love and believe in, and it will come naturally. -David Frost
Usilenge mafanikio kama unayataka, wewe fanya kile ambacho unapenda kufanya na amini kwenye kitu hiko na mafanikio yatakuja yenyewe.
Siku zote mafanikio yanakuja kw akufanya kitu ambacho unakipenda. Iwe ni kazi au biashara, hatua ya kwanza ya kufanikiwa ni kukipenda kile unachofanya.
SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha Megaliving -By Robin Sharma
Unapopenda unachofanya, unakuwa tayari kujitoa kwa moyo wako wote na unakuwa tayari kuweka juhudi, maarifa na ubunifu ili kutoa kilicho bora zaidi.
Unapotoa kilicho bora ndio unatengeneza njia ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Vipi kama hupendi unachofanya?
Unaweza kufanya mambo mawili.
1. Kipende.
2. Achana nacho na utafute kile unachopenda kufanya.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Siri Za Kuwa Mjasiriamali Bora Na Kufikia Mafanikio Makubwa.
Wednesday, April 15, 2015
NENO LA LEO; Jambo Muhimu La Kufanya Kila Siku Unapoamka Asubuhi.
When you arise in the morning, think of what a precious privilege it is to be alive - to breathe, to think, to enjoy, to love. -Marcus Aurelius
Unapoamka asubuhi, fikiria ni jinsi gani ulivyo na bahati ya kipekee kuwa hai – kupumua, kufikiri, kufurahia, kupenda.
SOMA; TABIA ZA MAFANIKIO; Umuhimu Na Jinsi Ya Kujijengea Tabia Ya Shukrani.
Kama huwezi kufurahia maisha yako kwa vile tu yalivyo unaweza kuwa na maisha magumu sana na maisha yako yatakwenda hivyo kwa muda mrefu.
Shukuru kwa maisha uliyonayo, kuwa hai ni zawadi ya kipekee kwako. Shukuru kwamba unaweza kupumua, shukuru kwamba unaweza kufikiri, shukuru kwamba umeweza kusoma hapa, shukuru kwamba unapenda na kuna wanaokupenda.
Usianze siku yako kwa kufikiria umekosa nini, kwa kufanya hivyo unakosa shukrani. Anza kwa kushukuru kwa vile ambavyo unavyo, ambavyo ni upendeleo mkubwa kwako.
Nakutakia siku njema.
Tuesday, April 14, 2015
NENO LA LEO; Hii Ndio Tiba Ya Muujiza Mkubwa.
Love is the great miracle cure. Loving ourselves works miracles in our lives. -Louise L. Hay
Upendo ndio tiba ya muujiza mkubwa. Kujipenda sisi wenyewe kunaleta miujiza mikubwa kwenye maisha yetu.
SOMA; Sababu Zinazokufanya Wewe Kushindwa Kuthubutu Wazo Lako
Kama una changamoto zozote kwenye maisha yako, kama una matatizo yoyote kwenye maisha yako, hebu anza kw akujipenda wewe mwenyewe kwanza.
Unapojipenda mwenyewe, kwanza unajiepusha na matatizo mengi ambayo yangeendelea kukusumbua. Na pia utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.
Upendo ni tiba kubwa sana na inayoweza kutenda miujiza mikubwa. Unapojipenda mwenyewe, utayathamni maisha yako, utakuwa na udhubutu na utaweka juhudi na maarifa ili uweze kupata kile unachotaka.
Unapojipenda mwenyewe pia inakuwa rahisi kwako kuwapenda wanaokuzunguka.
Jipende wewe kwanza na mambo mengine yatakwenda vizuri.
Nakutakia siku njema.
Monday, April 13, 2015
NENO LA LEO; Hiki Ndio Kipimo Cha Upendo.
The degree of loving is measured by the degree of giving. -Edwin Louis Cole
Kiwango cha upendo kinapimwa kwa kiwango cha kutoa.
Tunapima kiwango cha mtu cha upendo kwa kiwango ambacho yupo tayari kutoa. Upendo sio maneno, bali ni matendo.
SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.
Ni kiasi gani unampenda mtu itaonekana kwa kiasi ambacho upo tayari kujitoa kwa ajili yake.
Kama kweli unawapenda watu, onesha upendo wako kwa kujitoa kwa ajili yao.
Na kutoa sio fedha tu, bali kujali, muda, ushauri na mengine mengi ambayo yanaweza kumsaidia mtu kuondoka katika hali moja na kwenda kwenye hali nyingine.
Je kuna watu ambao unawapenda? Hebu jitoe kwa kuwatumia ujumbe huu, utawasaidia kuwa na msingi mzuri wa upendo.
Sunday, April 12, 2015
NENO LA LEO; Usiweke Maanani Unachoambiwa Na Mtu Aliye Kwenye Hali Hizi Tatu.
It's useless to hold a person to anything he says while he's in love, drunk, or running for office. -Shirley MacLaine
Haina maana kumwajibisha mtu kwa chochote anachosema wakati yuko kwenye mapenzi, amelewa au anagombea.
Katika hali hizi tatu, mtu anaweza kusema jambo lolote hata kama hana uywezo wa kulitekeleza
Mtu aliyepo kwenye penzi zito anaweza kuahidi mambo mengi sana lakini baadae akashindwa kuyatekeleza. Huenda hakuwa anamaanisha ila msukumo wa penzi ulimsukuma afanye hivyo.
SOMA; Hizi Ndio Siri 21 Za Mafanikio
Mtu aliyelewa hii iko wazi, ulevi huwafanya watu waseme mambo ambayo hawajayafikiria kwa kina. Ulevi huathiri uwezo wa mtu wa kuchambua mambo.
Mtu anayegombea nafasi yoyote naye anakuwa kwenye hali ya kutamani sana kushinda. Ili aweze kutimiza hilo yupo tayari kuahidi chochote ili iwe hivyo. Angalia wanasiasa wetu ni vitu vingpi wamekuwa wanaahidi wakati wa uchaguzi na ni vingapi wanatekeleza.
Kwa kujua kwamba mtu yeyote katika makundi haya matatu anaweza kusema jambo ambalo hamaanishi itafanya maisha yako kuwa rahisi kwa kutokuweka matagemeo makubwa kwa watu hawa.
Nakutakia siku njema.
Saturday, April 11, 2015
NENO LA LEO; Hiki Ndio Unachotakiwa Kufanya.
Only do what your heart tells you. -Princess Diana
Fanya kile ambacho moyo wako unakuambia ufanye.
Maisha ni yako na kama unataka kuyafurahia ni lazima ufuate kile moyo wako inachokuambia.
Kuna vitu ambavyo unapendelea kufanya hivi ndivyo vitakavyokuletea mafanikio. Kuna vitu ambavyo unajua ni muhimu kwako, vifanye hivi bila ya kusita.
Lakini kama utaacha kufanya kile moyo wako unakuambia na kuanza kufanya kile ambacho kila mtu anafanya utaishi maisha ambayo huyafurahii. Utakuwa unaishi maisha ya kuendeshwa na wengine na huwezi kujitofautisha na kufikia mafanikio.
Fanya kile ambacho moyo wako unakuambia ufanye, hiko ndio kina mafanikio makubwa kwako.
Nakutakia siku njema.
Friday, April 10, 2015
NENO LA LEO; Kinachofanya Maisha Yawezekane Na kinachoyafanya Yawe Rahisi.
Faith makes all things possible... love makes all things easy. -Dwight L. Moody
Imani inafanya kila kitu kiwezekane…. mapenzi(upendo) unafanya kila kitu kiwe rahisi.
Kama huna imani utaona kila kitu hakiwezekani hasa kwenye dunia hii ambayo imejaa kila aina ya changamoto, ni imani pekee itakayokuwezesha wewe kuendelea na mapambano licha ya kukutana na vikwazo. Amini kwamba unaweza, amini kwamba inawezekana na hakuna kitakachokuzuia kupata kile unachotaka.
SOMA; Huu Ndio Mtaji Mkubwa Ambao Tayari Unao.
Kama hakuna upendo, hakuna mapenzi maisha yatakuwa magumu sana. Upendo unatufanya tuweze kuwathamini wengine na wao kututhamini pia. Ni katika njia hii tunaweza kusaidiana na kuyafanya maisha kuwa rahisi sana. Mpende kila anayekuzunguka, jipende wewe mwenyewe na kubali pale wengine wanapokupenda. Hii ni zawadi pekee kwenye maisha ambayo haiangalii una nini, bali inakuangalia wewe kama wewe.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Hiki Ndio Kitu Kitakachokuletea Mafanikio Ambacho Tayari Unacho.
Thursday, April 9, 2015
NENO LA LEO; Siri Itakayokuwezesha Kufanya Chochote.
Love yourself first and everything else falls into line. You really have to love yourself to get anything done in this world. -Lucille Ball
Jipende wewe kwanza na vitu vingine vyote vitakwenda sawa. Unahitaji kujipenda mwenyewe ili uweze kukamilisha chochote hapa duniani.
Kama hujipendi wewe mwenyewe basi hakuna jambo kubwa unaloweza kufanya kwenye maisha yako. Utajidharau na kujiona hufai.
Lakini unapojipenda mwenyewe utajithamini na kujipa moyo kitu ambacho kitakupa hamasa ya kuweza kufanya jambo lolote unalotaka kufanya.
Jipende wewe mwenyewe kwanza, hii ndio siri kubwa ya kukuwezesha kufikia mafanikio.
Nakutakia siku njema.
SOMA; Tabia Hizi Zitakusaidia Sana Kufikia Malengo Yako Kwa Haraka - 2
Wednesday, April 8, 2015
NENO LA LEO; Hiki Ndio Kitu Muhimu Sana Kwenye Maisha Yako. Na Sio Chakula Au Hewa.
A flower cannot blossom without sunshine, and man cannot live without love - Max Muller
Ua haliwezi kuchanua pasipokuwepo na mwanga wa jua na mtu hawezi kuishi pasipokuwepo na upendo.
Upendo ni kiungo muhimu snaa cha maisha yetu. Bila ya upendo maisha yanakuw amagumu san akuishi na hata kufurahia.
Unaweza kupata chakula, unaweza kupata hewa unawez akuwa na fedha za kukutosha ila ukikosa upendo maisha yako yanakosa maana. Na utakuwa upo tu unasukuma siku lakini sio kwamba unaishi.
Upendo ni sehemu muhimu sana kwenye maisha yetu. Anza kwa kutoa upendo na utapokea mwingi mpaka utashangaa.
SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.
Tuesday, April 7, 2015
NENO LA LEO; Unachopata Kwenye Kupendwa Na Unachopata Kwenye Kupenda.
Being deeply loved by someone gives you strength, while loving someone deeply gives you courage. -Lao Tzu
Kupendwa sana na mtu mwingine kunakupa wewe nguvu, kumpenda sana mtu mwingine kunakupa wewe ujasiri.
Haitoshi tu wewe kusema kwamba unapendwa, unahitaji kupenda pia. Wapende wale wanaokupenda na hata wasiokupandea pia. Hakuna chochote unachopoteza kwa kumpenda mtu.
Dunia ingekuwa sehemu nzuri sana ya kuishi kama wote tungependana kama ndugu wamoja, kama binadamu sawa.
SOMA; Kauli KUMI Za Kukuhamasisha Kutoka Kwa Martin Luther King
Tunaporuhusu tofauti ndogo ndogo kama rangi, kabila na dini kutugawa, tunatoa nafasi ya kujiangamiza sisi wenyewe. Upendo ndio dawa ya matatizo yote uliyonayo kwenye maisha yako. Upendo ndio dawa ya matatizo yote tuliyonayo duniani.
Anza kujipenda wewe mwenyewe halafu wapende na wengine pia. Tutajenga dunia iliyo bora.
Mimi nakupenda sana wewe, nimekupa ujumbe huu mzuri, tafadhali utume kwa watu watano ambao unawapenda sana na wao wautume kwa wengine watano wanaowapenda(kama na mimi ni mmoja wa hao unaowapenda weka email yangu pia, makirita@kisimachamaarifa.co.tz). Na sisi sote tutakuwa mabalozi wa kusambaza upendo. Tafadhali sana usiuzuie upendo huu, usambaze na tuiponye dunia, KWA UPENDO.
Nakutakia siku njema.



