Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, January 6, 2015

UKURASA WA 06; Kazi Ndio Msingi Wa Maendeleo.

Tokea enzi na enzi za kuwepo kwa dunia haijawahi kutokea watu wakapata kila wanachotaka bila ya kufanya kazi. Hata wakati ambao watu waliishi kwa kula vyakula vya asili bado ilimbidi mtu kwenda kuwinda au kuzunguka msituni kutafuta mboga, matunda na vyakula vingine.

Lakini kwa njia moja au nyingine dunia ya sasa tumekuwa tukidanganyana kwamba unaweza kupata mafanikio bila ya kufanya kazi. Yaani unaweza tu kusheza kamari, ukabashiri kwamba timu fulani itashinda na hatimaye ukapata mamilioni, huu sio ukweli kabisa.

Pia dunia ya sasa watu wametingwa sana na kutafuta njia ya mkato ya kufikia mafanikio. Watu wanafanya mambo ya ajabu ili tu waweze kufikia mafanikio.

Ukweli ni kwamba hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio. Hakuna njia yoyote unayoweza kutumia kupata mafanikio bila ya kufanya kazi. Na kama njia hizi zipo basi haziwezi kukufikisha mbali.

Tambua kwamba ili uweze kuboresha maisha yako kwa mwaka huu 2015 inabidi ufanye kazi kwa juhudi na maarifa. Ni lazima jasho likutoke hata kama kazi unayofanya sio ya kutumia nguvu. Ni muhimu sana upende kile unachofanya na kukifanya kwa moyo mmoja. Kwa njia hii itakuwa rahisi kwako kufikia mafanikio.

TAMKO LA LEO;

Natambua ya kwamba njia pekee ya kufikia mafanikio ni kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, hakuna mbadala wa hapo. Nitatumia muda wangu vizuri mwaka huu 2015 ili niweze kufanya kazi zangu kwa ubora wa hali ya juu. Sitapoteza muda wangu kutafuta njia ya mkato ya kufikia mafanikio.

Tukutane kwenye ukurasa wa saba kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

 

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment