Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Showing posts with label MBINU ZA MAISHA. Show all posts
Showing posts with label MBINU ZA MAISHA. Show all posts

Friday, April 10, 2015

ELIMU SIO UFUNGUO WA MAISHA; Hiki Hapa Ndio Ufunguo Halisi Wa Maisha.

Hakuna anayekataa kwamba elimu ni muhimu sana tena sana. Na elimu zote mbili yaani rasmi na isiyo rasmi ni muhimu sana ili kuweza kuyakabili mazingira yetu, kupambana na changamoto tunazokutana nazo na hata kuboresha maisha yetu. Elimu ni muhimu kwa ajili ya kufikia maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Lakini ELIMU SIO UFUNGUO WA MAISHA ila elimu inakuwezesha wewe kuweza kuutumia vizuri ufunguo wa maisha.
Ufunguo wa maisha ni ule uwezo mkubwa ambao upo ndani ya kila mtu, ni kile kipaji ambacho mtu anaweza kukitumia kufanya mambo makubwa sana na kwa bahati mbaya sana elimu haimpatii mtu kitu hiki na wakati mwingine inakiua kabisa.
Ingelikuwa elimu ni ufunguo wa maisha basi tungetegemea kila mtu aliyesoma awe na maisha bora sana tofauti na yule ambaye hajasoma. Lakini huu sio uhalisia, watu wengi wamesoma ila na wengi pia wana maisha magumu kuliko hata wale ambao hawajafikia kiwango kikubwa cha elimu.
Nasisitiza tena elimu ni muhimu sana lakini kama hujaujua ufunguo wa maisha yako ni nini elimu haiwezi kukupatia kitu hiko. Unahitaji kujua ni nini ambacho kipo ndani yako na ni jinsi gani unaweza kukiboresha kwa elimu ambayo utaipata. Kama utaendelea kuamini kwamba elimu ndio ufunguo wa maisha utashindwa kugundua kile hasa kilichopo ndani yako na kufikiri kwa kupata elimu tu kila kitu kitakwenda vizuri.
Tunaishi kwenye dunia ambayo changamoto ni nyingi sana, kazi ni ngumu kupatikana na biashara zina changamoto nyingi kwa sababu kila mtu anaweza kufanya biashara zinazofanyika. Kitakachomfanya mtu aonekane sio tu elimu aliyonayo, maana sasa hivi karibu kila mtu ana elimu kubwa, bali ni kipi cha ziada ambacho mtu unacho na hapa ndio UFUNGUO WA MAISHA unapoingia.
Hivyo basi ni wakati wa kile mmoja wetu kujua ufunguo wa maisha yake ni nini na kutumia elimu aliyopata kuweza kuutumia vizuri ufunguo huo ili aweze kuboresha maisha yake na kufikia mafanikio makubwa.
TUPO PAMOJA.
Coach Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Sunday, April 5, 2015

Salamu Za Sikukuu Kutoka AMKA CONSULTANTS Na Mambo Muhimu Kwako Kuzingatia.

Leo ni sikukuu ya pasaka ambapo wakristo wote duniani wanaadhimisha mateso na kufufuka kwa mwokozi wao Yesu Kristo. Vile vile leo ni siku ya mapumziko kwa Watanzania wote.

Kampuni ya AMKA CONSULTANTS ambayo ndio inasimamia mitandao hii AMKA MTANZANIA, KISIMA CHA MAARIFA, MAKIRITA AMANI NA JIONGEZE UFAHAMU inachukua nafasi hii kukutakia wewe mtanzania sikukuu njema na mapumziko mema pia.

Katika sikukuu hii umekuwa na siku nyingi za mapumziko na kusherekea pia. Sherekea sikukuu hizi kwa amani na upendo na kumbuka kwamba kuna maisha baada ya sikukuu hizi.

Pia katika muda huu mrefu wa mapumziko, kumbuka kupata muda wa kufanya jambo ambalo ni muhimu kwako na ambalo hukupata muda wa kulifanya katika siku za kawaida.

AMKA CONSULTANTS itaendelea kuwa nawe katika safari ya kuboresha maisha yako. Lengo letu ni kufanya kazi na watu ambao wapo tayari kuchukua hatua ya kuboresha maisha yao na kuwasaidia kufikia lengo lao hilo. AMKA CONSULTANTS tunajua kwamba unawez akubadili maisha yako kama utakuwa tayari na kama ukipata msaada wetu ambao ni muhimu sana kwako.

Tutaendele akuwa nawe katika kila hatua ya maisha yako, kazi yako na hata biashara yako.

Endelea kutembelea mitandao yetu kila siku ili kujifunza, kuhamasika na kushauriwa. Tunakuahidi kupata huduma bora sana kulingana na mahitaji yako.

Karibu sana tufanye kazi pamoja.

Nawatakia watanzania wote sikukuu njema na mapumziko mema.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Mkurugenzi, AMKA CONSULTANTS.

N;B Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

Wednesday, April 1, 2015

MIAKA MIWILI YA AMKA MTANZANIA; Kwa Nini Ipo Na Itaendelea Kuwepo Na Mambo Mazuri Yanayokuja.

Tarehe 31/03/2013 ilikuwa ndio siku ya kwanza kwa makala ya kwanza kwenda hewani kwenye mtandao huu wa AMKA MTANZANIA. Kipindi hiko wakati naanzisha mtandao huu mambo hayakuwa kama sasa, watu walikuwa na muamko mdogo wa kusoma habari za aina hii na hata kujisomea vitabu. Leo hii miaka miwili tu mbele, mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana

Leo hii, miaka miwili baadaya kuanzishwa kwa mtandao huu nimeona ni vyema tukashirikishana kwa nini mtandao huu upo, utaendelea kuwepo na mambo makubwa yanayokuja.

Moja ya makala za mwanzo kabisa kwenye AMKA MTANZANIA;

UTARATIBU WA KUJISOMEA VITABU

USIMLAUMU YEYOTE, ANZA KUJILAUMU WEWE

ZOEZI ZURI LA KUFANYA KILA SIKU

Kwa nini mtandao huu upo?

Miaka miwili kabla ya kuanz akwa mtandao huu, nilikuwa naishi kwenye hadithi nzuri ambayo tumekuwa tukidanganywa. Hadithi kwamba nenda shule, soma kwa bidii, faulu vizuri na utapata kazi nzuri na kuwa na maisha mazuri. Nilisoma kwa bidii kweli na kufaulu vizuri sana masomo yangu ya kidato cha sita. Baada ya hapo nilipata nafasi ya kusomea udaktari wa binadamu. Kwa nafasi hii niliamini ndio nimepata tiketi ya maisha mazuri.

Lakini mambo yalibadilika sana baadaya ya kuanza masomo haya ya udaktari. Baada ya kuona kile nitakachokwenda kufanya na mazingira ya kukifanya na hata maisha ya madaktari wengine, sikushawishika sana kama mwanzo kwamba kuwa daktari ndio tiketi ya maisha bora.

Changamoto kubwa zaidi ilitokea mwaka 2011 ambapo nilijikuta nje ya mfumo wa elimu, huku sina degree wala chochote cha kuniwezesha kupata kazi ya kujikimu kwenye maisha yangu. Mbaya zaidi hakuna aliyeweza kunielewa kwenye kipindi hiki kwa sababu kila mtu anayenifahamu aliona nimefanya makosa makubwa sana kwenye maisha, sijui ninachofanya na mengine mengi. Ni hapa ndio nilipoamua kushika hatamu ya maisha yangu. Nilikaa chini na kuamua kwamba kama nitakwenda kufanikiwa kwenye maisha yangu, basi hiyo ni juu yangu. Na nilijiambia kabisa kwamba mafanikio kwenye maisha hayahitaji degree au elimu yoyote kubwa.

Ni baada ya maamuzi haya ndipo niliacha kulalamika na kuanz akuchukua hatua juu ya maisha yangu. Nilitafuta kazi yoyote ninayoweza kufanya ili angalau iniwezeshe kuendelea kuwepo mjini. Nilipata kazi hiyo na sio kwa sababu ya kuwa nimesomea kazi hiyo, au kwa sababu ya kujulikana, bali kwa ushawishi niliokuwa nautoa kwenye maombi ya kazi hiyo.

Baada ya hapa niliamua kujifunza na kuangalia ni kitu gani ninachopendelea kufanya. Nilianza kujifunza mambo yanayohusiana na teknolojia ya habari(IT) ambapo nilijifunza jinsi ya kutengeneza tovuti, blog, programu za kompyuta na vitu vingine vingi. Yote haya sikuwa na darasa la kufundishwa, bali nilitafuta vitabu na kujisomea kisha kufanyia kazi yale ambayo nimeyasoma. Uzuri ni kwamba nilikuwa naona matokeo mazuri kila ninapojifunza na kufanya kitu.

Baada ya mwaka mmoja wa kujifunza vitu vya kitaalamu na pia kujisomea vitabu vyakujijenga na kujihamasisha niliona mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yangu. Kwanza nilijikuta katika hali kubwa ya kujiamini, nikiwa na vyanzo mbalimbali vya mapato kutoka kwenye shughuli mbalimbali ambazo nilikuwa naweza kufanya. Ni katika wakati huu ambapo niliona makosa makubwa niliyokuwa nafanya kwenye maisha yangu na jinsi nilivyoweza kuyarekebisha.

Ni wakati huu pia ambapo niliona watu wengi wanafanya makosa haya na kunafanya maisha yao yawe magumu sana. Ndio maana niliona kuna umuhimu wa kuwashirikisha vitu hivi vizuri ambavyo nimefanya kwenye maisha yangu na ninaendelea kuvifanya ili nao waweze kuboresha maisha yao. Hapa ndipo mtandao huu wa AMKA MTANZANIA ulipozaliwa. Lengo kubwa la mtandao huu ni kumsaidia kila mtanzania ambaye ameamua kushika hatamu ya maisha yake kuweza kufikia malengo na mipango aliyojiwekea kwenye maisha yake.

Kwa nini nimekushirikisha sehemu hiyo ndogo ya maisha yangu na historia ya mtandao huu?

Nimefanya hivi kwa sababu najua kuna kijana wa kitanzania ambaye amemaliza masomo yake ila hajapata ajira. Kijana huyu amekaa nyumbani na hajui afanye nini, kwani hata biashara anasema hana mtaji. Nataka kukuambia wewe kijana mwenzangu kwamba AMKA na uchukue hatamu ya maisha yako, utakapoamua kuamka hakuna linaoshindikana.

Najua kuna mfanyakazi ambaye amefanya kazi kwa muda mrefu sasa ila haoni kitu kikubwa ambacho amefanya kwenye maisha yake. Maisha yake yamekuwa ya kuamka, kwenda kazini, kurudi nyumbani na kesho pia kufanya hivyo. Kipato anachopata pia hakioni kwa sababu kinaishia kulipa madeni na kulipia gharama za maisha. Nataka kukuambia wewe mtanzania mwenzangu, haijalishi kazi yako ni ya chini kiasi gani, haijalishi umeifanya kw amuda gani, kuna njia nzuri sana za wewe kuweza kuyabadili maisha yako na kuwa bora sana zaidi ya sasa ambapo unayaona yanakwenda tu.

Pia najua kuna mfanyabiashara ambaye amekuwa anafanya biashara zake kwa muda mrefu ila haoni mabadiliko yoyote kwenye biashara hiyo. Au ameanza biashara na kupata hasara hivyo kuamini kwmaba biashara haiwezekani. Napenda kukuambia kwamba kuna mbinu nzuri sana za kufanya biashara zako na kama ukiamua kuzitafuta na kuzifuata maisha yako yatakuwa tofauti sana na yalivyo sasa.

Maisha yoyote ambayo unapitia sasa, hata yawe magumu kiasi gani, unayo nafasi kubwa sana ya kuyabadili wewe mwenyewe. Huna haja ya kulaumu serikali, kulaumu wazazi au kulaumu mtu mwingine yeyote unayefikiri ndio anakuletea maisha hayo magumu. Leo nakuambia kwamba, maisha magumu uliyonayo, yataondolewa na wewe mwenyewe.

Kwa nini AMKA MTANZANIA itaendelea kuwepo.

AMKA MTANZANIA itaendelea kuwepo kwa sababu bado watanzania wengi hawajaamka. Bado watanzania wengi wamekabidhi maisha yao kwa waajiri wao, kwa serikali, kwa jamii na wameruhusu taasisi hizi zifanye maamuzi muhimu kwenye maisha yao. Hii ndio maana wanaona maisha yao yakienda tu na hivyo kuishia kulaumu pale ambapo kile walichotarajia hakijatokea.

Bado watanzania tunahitaji maarifa muhimu sana ya kuweza kuboresha maisha yetu na kufanikiwa zaidi. Sehemu kubwa sana ya watanzania wanafanya mambo kwa mazoea. Wanafanya kazi kwa sababu ndio kazi ambayo wamekuwa wanaifanya kila siku. Wanafanya biashara kwa sababu wamezoea kufanya biashara hiyo. Hii ni sumu kubwa sana ya kufikia mafanikio makubwa kama unavyoweza kuisoma vizuri kwenye kitabu JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA.

Mtandao huu utaendelea kuwepo na kutoa makala na mafunzo mazuri yatakayomwezesha kila aliyeamua kuboresha maisha yake kuweza kufikia lengo hilo.

Mambo mazuri yanayokuja kwenye AMKA CONSULTANTS.

Ilianza AMKA MTANZANIA ambayo ilikuwa na jukumu kubwa la kukupa wewe taarifa muhimu unazohitaji kuwa nazo ili kuboresha maisha yako. Mwaka mmoja baadae ikaja KISIMA CHA MAARIFA ambayo ni sehemu maalumu kwa wale ambao wako tayari kufikia mafanikio makubwa sana kwenye maisha yao. Kupitia KISIMA CHA MAARIFA watu wanajifunza tabia za mafanikio, mbinu za kufikia mafanikio, biashara na ujasiriamali na hata kupata uchambuzi wa vitabu vizuri. Kupitia KISIMA CHA MAARIFA pia unapata nafasi ya kukutana na watanzania wengine ambao nao wanaelekea kwenye safari ya mafanikio.

Kuna mambo mengi na mazuri ambayo yataendele akukujia kupitia mtandao huu wa AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Endelea kutembelea mitandao hii na washirikishe wengi zaidi ili nao wapate mambo haya mazuri.

Kuna kipengele muhimu kitakachokuja kwenye AMKA MTANZANI ambapo tutapata shuhuda za watu mbalimbali ambao maisha yao yamebadilika sana baada ya kujifunza kupitia AMKA MTANZANIA na kuamua kufanyia kazi yale ambayo wamejifunza. Shuhuda zipo nyingi mpaka sasa. Kama na wewe ungependa kuwashirikisha watanzania wenzako ushuhuda mzuri kutokana na uliyojifunza kwenye mtandao huu tafadhali andika maelezo yako kwa kujitambulisha, kueleza ulipotoka, ulipo sana na unapokwenda na jinsi gani AMKA MTANZANIA imekusaidia kisha tuma kwenye email makirita@kisimachamaarifa.co.tz Tafadhali fanya hivi na utakuwa sehemu ya mabadiliko ya nchi yetu na watanzania wenzetu.

Ufanye nini ili maisha yako kuwa bora ziadi?

Kwanza kabisa chukua maamuzi juu ya maisha yako, jua kama utakwenda kufanikiwa basi ni kwa juhudi zako na hakuna atakayekuletea mafanikio hayo.

Pili amua kujifunza sana kuhusiana na hiko unachofanya na maisha yako kwa ujumla. Jisomee vitabu mbalimbali vinavyotumwa kwenye mtandao huu na endelea kusoma mtandao huu kila siku kwa sababu kila siku kunakuwa na makala nzuri za kukuwezesha kuboresha maisha yako.

Tatu, jiunge na KISIMA CHA MAARIFA, kwa kuwa ndani ya kisima utajifunza mbinu nyingi sana za kukuwezesha kufikia mafanikio na pia utapata nafasi ya kukutana na watanzania wengine ambao wameamua kuchukua hatamu ya maisha yao. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na weka taarifa zako kisha lipa ada ya uanachama na utapata nafsi ya kupata maarifa hayo adimu. Kuhakikisha unapata mambo yote mazuri lipia ada ya GOLD MEMBER.

Naomba nichukue nafasi hii kukushukuru sana wewe msomaji ambaye umekuwa na mtandao huu mpaka sasa. Ni kwa sababu yako ndio maana mtandao huu umeendelea kukua na kuwafikia wengi zaidi. Umekuwa ukiwashiriksiha wengine habari za mtandao huu na kuwafanya wautembelee pia. Tafadhali endelea kuw abalozi mzuri wa AMKA MTANZANIA na hakikisha kila mtu unayemfahamu naye amefahamu kuhusu mtandao huu ili na yeye autembelee na kujifunza.

Pia niseme kwamba sisi sote tunaendelea na safari ya kujifunza, hakuna anayejua zaidi bali tunajifunza na wakati mwingine tunafanya makosa. Mimi na waandishi wengine wa mtandao huu sio kwamba ndio mabingwa sana kwenye kile tunachoandika, ila tunapenda kujifunz ana kutumia mambo haya na maisha yetu yanakuwa bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda. Na wewe usikose nafasi hii ya kuboresha maisha yako kila siku hata kama ni kidogo kiasi gani.

Nakutakia kila la kheri katika kuboresha maisha yako. Kumbuka kwamba kila kitu kinawezekana kama ukiamua kuchukua hatua. Kama kuna jambo lolote ambalo linakupa changamoto na ungependa kupata ushauri zaidi karibu sana tuwasiliane. Unaweza kupiga simu kwenye namba 0717396253 na tukaona ni jinsi gani tunaweza kusaidiana kwenye jambo hilo.

TULIKUWA PAMOJA, TUPO PAMOJA NA TUTAENDELEA KUWA PAMOJA. Tafadhali tuma makala hii kwa njia ya email kwa watu watano na nicopy(weka email yangu makirita@kisimachamaarifa.co.tz kwenye sehemu ya cc) kwenye email hiyo na nitakutumia zawadi nzuri ya kitabu cha kufaidika na mabadiliko.

kitabu-kava-tangazo4322

Wednesday, February 25, 2015

Kama Unataka Kuitawala Siku Yako Ya Kesho Fanya Kitu Hiki Kimoja Kesho Asubuhi.

Unapoamka kesho asubuhi, usiamke kwa kujivuta vuta, wala usiamke kivivu vivu wala usianze kufikiria kama uamke au la.
Muda wa kuamka unapofika, LIPUKA kutoka kitandani.
Yaani lipuka kama bomu, na utaianza siku yako ukiwa na hamasa kubwa na nguvu kubwa.
Na kwa kuianza siku yako kwa mlipuko utaishangaza siku na dunia itakuogopa na kukupatia kile unachotaka.
Usiamke tu kinyonge, LIPUKA kutoka kitandani.

Sunday, February 1, 2015

Ni Muda Unaenda Haraka Au Wewe Unaenda Taratibu?

Kufumba na kufumbua mwezi wa kwanza hatunao tena...
Tuko mwezi wa pili na siku sio nyingi tutauanza mwezi wa tatu.
Ni majuzi tu tulikuwa tunasherekea mwaka mpya, sasa hivi ni kama umechakaa.
Muda unakwenda haraka eh?
Hiki ndio kila mtu anachosema, kwamba muda unakwenda haraka sana.
Lakini je ni kweli?
Ni kweli muda unakwenda haraka au sisi tunakwenda taratibu?
Kipimo cha muda tunachotumia ni kile kile ambacho tumetumia miaka mingi iliyopita.
Iwe ni kwa kutumia saa, machweo na mawio na hata mzunguko wa mwezi. Vyote hivi havbijabadilika.
Ila sisi tunaona mabadiliko, muda unakwenda haraka sana.
Kwa dhana hii ya kwamba vipimo vyetu vya muda havijabadilika, ni dhahiri kamba sisi ndio tunakwenda taratibu.
Na kama tusipogundua mapema tutazidi kubaki nyuma.
Tufanye hima, muda hautusubiri.

Saturday, January 31, 2015

Huu Ni Mwaka Wa Kuacha Unafiki...

Umefika wakati wa kuacha unafiki..
Maana kuendelea na unafiki huu hakuwezi kukusaidia tena.
Swali la msingi; wakati unazaliwa au unakua ni nani alikuambia maisha yatakuwa rahisi? Kwamba utapata kila kitu kwa urahisi? Kwamba kutakuwa na njia za mkato za wewe kupata unachotaka?
Hakuna popote umewahi kuambiwa hivi.
Lakini kwa unafiki umeamua kulalamikia mambo hayo.
Kwamba maisha ni magumu, kwamba hupati njia ya mkato ya kufikia mafanikio.
Achana na unafiki huu,
Maisha ni magumu ndio, lakini ugumu wa maisha ndio unayafanya yawe mazuri kuishi.
Hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio, na kutokuwepo kwa njia hii ndio kunafanya safari ya kuelekea kwenye mafanikio kuwa nzuri.
Furahia kila hatua ya maisha yako.
Jifunze kutokana na changamoto unazopitia.
Acha kulalamika.

Friday, January 30, 2015

Je Upo Tayari Kupata Unachotaka? Siri Ni Hii Moja…

Unataka nini kwenye maisha yako?

Maana kama hujui unachotaka tayari umeshakikosa.

Je upo tayari kupata hiko unachotaka?

Ni nini kinakuzuia mpaka sasa hujakipata?

Haya ni maswali muhimu sana ya kujiuliza. Maana kuna kitu ambacho kimekufanya mpaka sasa hujapata unachotaka na kushindwa kujua kitu hiko kitaendelea kukuzuia.

Jua kikwazo ni nini na anza kukishughulikia.

Anza na vikwazo hivi;

Kwa watanzania waliowengi, vikwazo vinafanana na baadhi ya vikwazo hivyo ni;

1. Kutokujiamini.

2. Hofu

3. Kulalamika

4. Kutegemea kuna mtu atakuja kukutoa hapo ulipo.

5. Matumizi mabaya ya hela.

6. Uvivu, kutokuwa na ubunifu. Kuiga

7. Kukosa uvumilivu na kukata tamaa mapema.

8. Kutafuta njia ya mkato

9. Kukosa uaminifu

10. Kupanga malengo na mipango ila kushindwa kuchukua hatua.

Anza kufanyia kazi mambo hayo kumi na utaona ilivyo rahisi kupata chochote unachotaka.

Thursday, January 29, 2015

Nafasi Ya Wewe Kuwa Bora Kila Siku… NA ZAWADI YA TSH 365,000/=

Kama mpaka sasa huna utaratibu wa kujifunza kila siku, tayari upo nyuma sana katika kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako.

Kujifunza kila siku ni hitaji la chini sana la wewe kuweza kufikia mafanikio. Na tunaposema kujifunza kila siku ni kila siku kweli, jumatatu mpaka jumapili na kurudia tena na tena na tena.

Pamoja na umuhimu wa kujifunza kila siku, bado tunaishi kwenye jamii ambayo haitupi nafasi kubwa ya kujifunza. Hii ni kutokana na kuzungukwa na mazingira yenye changamoto nyingi zinazozuia kujifunza kila siku.

Kutokana na changamoto hizi ndio kulikonisukuma kutumia muda wangu kukupatia wewe nafasi ya kujifunza zaidi. Kupitia blog ya MAKIRITA AMANI utaweza kupata nafasi ya kujifunza kila siku, jumatatu mpaka jumapili.

Kila siku utaianza siku yako kwa neno la siku, hili ni neno ambalo litakupa hamasa ya kuweza kuifanya siku yako kuwa bora zaidi. Na pia kila siku kwa mwaka huu 2015 utapata ukurasa mmoja katika safu ya kurasa 365 za mwaka 2015. Kama bado hii haitoshi, unapata nafasi ya kupata kauli za kuhamasisha kutoka kwa viongozi na watu mashuhuri ambao wamefanikiwa sana. Na pia utaweza kupata hadithi za mafunzo ambapo utawez akujifunz akupitia visa mbalimbali.

Pamoja na haya yote utakuwa ukipata makala zenye fikra za kukuchokoza. Hizi ni zile ambazo zinaniingia kwenye fikra zangu kutokana na mawazo mbalimbali yanayonifikia katika kutafuta njia za kufanya maisha yangu na ya wewe msomaji kuwa bora zaidi kila siku.

Kwa kifupi wewe kutembelea blog hii ni sawa na kuwa na mimi pembeni yako, kwani utapata kitu kizuri kutoaka kwangu pale unapokihitaji.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za mbalimbali za kukufundisha na kukuhamasisha kila siku bonyeza hapa na uweke email. Kila siku kwenye email yako utapata mambo haya moja kw amoja.

Siku yako itakuwa bora sana kwa kuwa karibu na blog hii nzuri kwako.

Kama ningekuwa natoza wasomaji fedha kulingana na elimu ninayoitoa hapa, kila msomaji angetakiw akulipa tsh elfu moja kila siku. Hivyo kwa mwaka ungetakiw akulipa tsh 365,000/= ili kupata elimu hii muhimu sana kwako. Lakini sijataka wewe uingie gharama yoyote, gharama yako ni wewe kufungua blog, kusoma makala na kufanyia kazi yale unayojifunza.

Ombi moja muhimu sana kwako ni wewe kuwaalika watu wengi zaidi kusoma blog hii. Haina gharama yoyote na wala haitakuja kuw ana gharama yoyote. Tafadhali tuma makala hii kwenye email za watu watano, itume kama ilivyo halafu nikopy kwenye email hiyo utakayotuma, tumia email makirita@kisimachamaarifa.co.tz kama hujui jinsi ya kukopi, wakati unaweka email ya unayemtumia chini yake kuna cc, hapo weka email yangu. Na mimi nitakupa zawadi nzuri sana ya kitabu cha mabadiliko ambacho bado nakiandika.

Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya kuboresha maisha yako.

TUPO PAMOJA SANA.

 

Wednesday, January 28, 2015

Hii Ndio Sababu Kwa Nini Watu Wanafurahia Pale Unapoanguka...

Ukweli ni kwamba, pale unapoanguka au kushindwa watu wanafurahia sana.
Unaweza kuona sio kweli lakini ndio hali halisi ilivyo.
Watu wengi wanaokuzunguka wanaweza kufurahia sana pale unapofanikiwa. Lakini pia unapoanguka kuna watu wanaofurahia sana.
Hawafurahii kwa sababu wanakuchukia wewe ila maisha yao ndio yanawalazimisha kufurahia hali hiyo.
Watu wengi wana maisha magumu sana, hivyo wakiona kuna mtu mwingine ana maisha magumu zaidi yao wanapata ahueni, kwamba angalau na wao hawako wenyewe.
Hii inawafanya wafurahi na hii inatokea kisaikolojia bila hata ya kulazimisha.
Hujawahi kuona mtu anamweleza mwenzake mataizo halafu wanaanza kushindana ni nani mwenye matatizo mengi?
Unamwambia mtu mimi nina matatizo kweli, sina fedha, nina mgonjwa, na kazi/biashara haziendi vizuri. Yeye anakwambia hunifikii mimi, sina hela kabisa, watoto wanahitaji ada na kazi sina.
Ukweli ni kwamba kila mmoja kati yenu anakuwa anafurahia kwamba sio yeye tu ana matatizo.
Unapoingia kwenye matatizo, jitahidi uweze kuyatatua na usonge mbele, wengi wa watakaokuwa wanakupa moyo wanafurahia wewe kuwepo kwenye matatizo hayo.

Tuesday, January 27, 2015

Unataka Kujifunza Kitu Chochote Unachoona Ni Kigumu? Fanya Hivi...

Njia bora kabisa ya kujifunza ni kufanya, kutenda.
Utasoma vitabu vyote, utafundishwa na walimu waliobobea ila kama hutatendea kazi yale uliyojifunza ni kazi bure.
Hakuna mtu aliyewahi kujifunza na akajua kuendesha baiskeli kwa kusoma vitabu tu. Hata baada ya maelekezo ulihitaji kuipanda baiskeli, kuanguka na hata kuumia ndio ukajua kuendesha baiskeli.
Sasa nini kinakuzuia wewe kuchukua hatua sasa? Hujajifunza? Anza kufanya.
Unataka kujifunza biashara, anza kufanya biashara, anza kidogo kidogo.
Unataka kujifunza kuandika makala nzuri anza kuandika, anza maneno matano nenda kumi, ishirini, mia...
Unataka kujifunza kilimo, nenda tafuta shamba, anza kulima.
Unataka kujifunza maisha, anza kuishi, sio kuishi kama kila mtu anavyoishi, bali kuishi kama ambavyo unataka kuishi.
Mwaka huu ni JUST DO IT.
Chochote unachotaka kwenye maisha yako, anza kukifanyia kazi. Hakuna kitakachokushinda.

USHAURI ADIMU; Usijenge Nyumba Kwenye Uwanja Wa Kukodi.

Usijenge nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi.
Inaonekana rahisi sana kusema hivyo, na hivi kweli unaweza kufanya hivyo?
Yaani mtu kakudoshishia uwanja wake, ufanyie shughuli zako kwa siku chache wewe ukaamua kujenga kabisa nyumba ya kudumu?
Kwa akili ya kawaida huwezi kufanya hivyo, kwa sababu unajua unakaribisha matatizo. Mwenye uwanja wake akiutaka nyumba yako inakuwa haina thamani tena. Na hata ukisema utaununua uwanja huo, wakati umeshajenga atakutajia bei anayotaka yeye kwa sababu anajua huna yena ujanja.
Sasa ni wapi ambapo unajenga nyumba kwenye uwanja wa kukodi?
1. Unapofanya biashara na mteja wako akawa mmoja, mteja huyu anaweza kuitikisa biashara muda wowote.
2. Unapoajiriwa na kutegemea ajira kwa maisha yako yote. Hata kama ajira itakusumbua hutaweza kuondoka maana maisha yako yanategemea hapo.
Usikubali kabisa kujenga nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi.
Unafanyaje sasa kama tayari umeshajenga nyumba kwenye uwanja wa kukodi?
Rahisi, nunua uwanja mwingine na anza kujenga nyumba yako.
Kama unafanya biashara inayokufunga anza kuipanua biashara hiyo.
Kama upo kwenye ajira unayoitegemea kwa asilimia 100 kwa kipato, anza kutengeneza vyanzo vingine vya kipato.
Bado hujui unawezaje kutanua biasara yako zaidi? Au hujui ni jinsi gani unaweza kutengeneza kipato cha ziada nje ya mshahara? Haya unaweza kujifunza kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Tembekea www.kisimachamaarifa.co.tz
Nakutakia kila la kheri.
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Monday, January 26, 2015

Yako Wapi Yale Maisha? Ni Wakati Wa Kulipa Deni Sasa.

Kila mtu alipokuwa mdogo alikuwa na picha kubwa sana ya maisha yake.

Ulipokuwa mdogo mtu akikuuliza unataka kuwa nani ulikuwa unajibu bila ya wasi wasi wowote kile unachotaka kuwa.

Ulikuw ana picha kubwa ya maisha yako, vile unataka yawe na kile unachotaka kutoa.

Safari ikaendelea na mahala fulani mambo yakabadilika.

Ukaanza kuambiwa hiki hakiwezekani, huwezi hiki, huna hiki, acha kuota na kadhalika.

Maneno haya uliyapuuza mwanzoni, ila yaliendelea kila siku, ukajaribu kufanya licha ya maneno haya, ukashindwa.

Na hapa ndio kitu kibaya sana kilichotokea, baada ya kushindwa tu, ukakubaliana nao, kwamba walikuwa sahihi, kwamba wewe huwezi, kwamba wewe huna, kwamba wewe unaota ndoto za mchana.

SOMA; Njia 12 za kurahisisha maisha yako.

Na sasa hatimaye unaishi maisha anayoishi kila mtu, huyafurahii lakini unaenda nayo tu, kwa sababu wanazidi kukuambia kwamba hiki ndio ulichopata, shukuru, huwezi kupata zaidi ya hiko.

Huu wote umekuwa ni uongo mkubwa sana uliojazwa kwenye kichwa chako. Wazazi na jamii zimejitahidi kukujengea uwezo huo, mfumo wa elimu ukamalizia kabisa na sasa unaona ndivyo mambo yalivyo.

Sasa leo jiulize swali moja…

Yako wapi yale maisha?

Tatizo letu binadamu ni kwamba kama hatujapata kile tunachokitaka kweli mioyo yetu haiwezi kutulia. Utafanya kila kitu ili kujiridhisha kwamba maisha ni mazuri lakini bado utakuwa na deni. Utajaribu kujiweka kwenye mazingira ya kuonekana una mafanikio kwenye maisha, lakini unapokaa chini na kutafakari maisha yako, utaona kuna deni fulani lipo ndani yako.

Sasa ni wakati wa wewe kulipa deni hilo.

SOMA; Kama Ulikuwa Hujui Bahati Inavyopatikana Soma Hapa.

Maswali muhimu wewe kujiuliza ni;

Je naridhishwa na kazi au biashara ninayofanya sasa?

Je naridhishwa na aina ya maisha ninayoishi sasa?

Je natoa mchango wa maana kwa kile ninachofanya kwenye jamii yangu na dunia kwa ujumla?

Je ningekuwa na uhakika nina mwezi mmoja tu wa kuishi, ningeutumia mwezi huo kufanya nini?

Maswali hayo yatakufungua ujue deni ambalo bado unadaiwa. Ukiweza kulipa deni hili maisha yako yatakuwa ya furaha hata kama huna utajiri mkubwa.

Huu ni wakati wa wewe kulipa deni. Jibu maswali hayo na chukua hatua.

Uzuri ni kwamba kwenye maisha hakuna kuchelewa. Katika wakati wowote ambao umegundua kwamba njia uliyokuwa unaenda siyo, unaweza kuibadili na ukaboresha maisha yako.

Nakutakia kile la kheri,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

SOMA; Hii Hapa Ni Tsh 604,000/= Utakayokabidhiwa Leo Usiku. Utaitumiaje?

Sunday, January 25, 2015

Kitu Muhimu Cha Kufanya Kabla Ya Kutumia Muda Au Fedha.

Muda una thamani kubwa sana kuliko fedha, hii ni kwa sababu ukipoteza fedha unaweza kupata nyingine ila ukipoteza muda huwezi kuupata tena.
Ila muda na fedha vina tabia moja inayofanana, ukivitumia bila ya kuandika kwenye karatasi unavipoteza.
Kitu muhimu cha kufanya kabla ya kutumia fedha au muda ni kupangilia matumizi hayo kwa kuandika kwenye karatasi au kitabu.
Usipopangilia kwa kuandika, utajikuta umetumia hovyo na hivyo kupoteza muda wako au fedha zako.
Weka mipango kabla ya kutumia muda au fedha.
Itakusaidia kuvitumia vitu hivyo viwili kwa makini.

Saturday, January 24, 2015

Jambo Moja La Kushangaza Kuhusu Maisha.

Jambo la kushangaza kuhusu maisha ni kwamba kila mtu anajua ni jinsi gani maisha ya mwenzake inabidi yawe ila hajui yakwake yanatakiwa kuwaje.
Ndio maana ni rahisi sana mtu kutoa maoni kwa mtu kwamba anakosea au hajui anachofanya, wakati maisha ya huyo mtoa maoni pia yanahitaji marekebisho.
Usianguke kwenye hili, hakikisha maisha yako yanakuwa kipaumbele kwako.

Friday, January 23, 2015

Jibu Swali Hili Na Fanyia Kazi Jibu Lako, Maisha Yako Yatabadilika Sana.

Hili ni swali la msingi sana ambalo kama ukiweza kujiuliza na ukajijibu kwa uaminifu basi maisha yako yatabadilika na kuwa bora sana.
Msisitizo ni jibu kwa uaminifu na fanyia kazi majibu yako.
Swali lenyewe ni hili;
KAMA UNGEWEZA KUWA BORA SANA DUNIANI KWENYE KITU KIMOJA TU, UNGECHAGUA KITU GANI?
Andika jibu lako mara moja na anza leo hii kufanyia kazi na siku moja utaikumbuka siku ya leo na kushukuru sana hatua uliyochukua.
Kama umekwama na hujui wapi pa kuanzia niandikie email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz
KILA LA KHERI.

Wednesday, January 21, 2015

Kama Sio Wewe Nani? Kama Sio Sasa Lini?

Kama sio wewe utakayebadili maisha yako unafikiri ni nani atakayefanya hivyo?
Kama sio sasa utabadili maisha yako umafikiri ni lini utafanya hivyo?
Usijidanganye kwamba kuna mtu atakayekuja kukutoa hapo ulipo, ni lazima nia hii itoke ndani yako.
Usijidanganye kwamba utabadili maisha yako kesho, kesho haijawahi kufika.
NI WEWE, NI SASA,
CHUKUA HATUA YA KUBADILI NA KUBORESHA MAISHA YAKO SASA.

Tuesday, January 20, 2015

Kuna Makundi Matatu Ya Watu; Je Wewe Upo Kwenye Kundi Lipi Kati Ya Haya? Fungua Kujua.

Duniani kuna makundi matatu ya watu. Na watu wote duniani tunaingia kwenye moja wapo ya makundi haya.

Kundi ulilopo linaweza kuw akiashiria kama utafikia mafanikio au la.

Na habari njema ni kwamba unaweza kubadilisha na kwenda kwenye kundi jingine ambalo litakufikisha kwenye mafanikio unayotaka.

SOMA; Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.

Makundi hayo ni kama ifuatavyoShifty

1. Kuna watu ambao wanaangalia mambo yakitokea na hawafanyi lolote.

2. Kuna watu ambao wanashangaa mambo yametokeaje.

3. Kuna watu ambao wanafanya mambo yanatokea.

Sasa wanaofikia mfanikio makubwa nadhani utakuwa umeshajua ni kundi lipi; ni wale wanaofanya mambo yanatojea.

Kwa hiyo kama na wewe ukiamua kufanya mambo yatokee, uache kuwa mtazamaji tu au uache kushangaa utafikia mafanikio yoyote unayotazama.

Kumbuka 2015… JUST DO IT.

SOMA; Kauli Mbiu Ya Mwaka Huu; JUST DO IT.

Monday, January 19, 2015

Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Binadamu tunapenda kulalamika sana na hata kuwalaumu wengine. Hakuna mtu anayependa aonekane kwamba yeye ndio amechangia kusindwa kwa jambo fulani. Hivyo katika jambo lolote lile linalotokea watu hukimbilia kumtafuta mchawi, yaani mtu wa kulaumu.

SOMA; Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku.

Sasa kwa tabia hii ya kulalamika na kulaumu inakurudisha sana wewe nyuma katika maendeleo ya maisha yako.

Huwezi kufikia mafanikio kama kila mara wewe ni mtu wa kulalamika na kulaumu wengine.

Leo hii nataka ufanye changamoto moja ambayo itakuwezesha kuondokana na tabia hii ili uweze kufikia mafanikio.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Kwa siku kumi kuanzia leo, jiepushe kulalamika au kumlaumu yeyote. Hakikisha siku nzima imesiha bila ya kulalamika au kulaumu. Ikitokea umefanya siku ya kwanz aila ya pili ukajisahau na kulalamika, unafuta na kuanz atena upya. Endelea hivi mpaka siku kumi ziishe bila ya kulalamikia kitu chochote.

Pia katika siku hizi kumi usimseme mtu kwa jambo lolote baya, yaani usisengenye, usishiriki majungu na wala usifanye umbea. Hizi ni tabia ambazo zinakurudisha sana nyuma.

SOMA; Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

Fanya changamoto hii na kama ukifanikiwa kukamilisha siku kumi nitumie email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz kunijulisha umeionaje hali hiyo na pia nitakuwa na zawadi nzuri kwako.

Na changamoto ianze, tutakutana upande wa pili, KARIBU SANA.

Sunday, January 18, 2015

Jambo Muhimu La Kufanya Leo Jumapili Usiku.

Jumapili ndio inaisha na kesho tunaanza wiki nyingine mpya.
Kuna mambo mengi unaweza kufanya siku ya leo kabla haijaisha.
Ila kuna jambo moja muhimu sana ambalo kama utashindwa kulifanya unaweza kupoteza wiki yako nzima.
Jambo muhimu la wewe kufanya leo ni kuipangilia wiki yako.
Jua ni mambo gani ambayo utahitaji kukamilisha kwenye wiki inayoanza kesho. Jua kila kitu utakachofanya kabla wiki haijaanza.
Kwa njia hii utakuwa na matumizi mazuri ya muda wako.
Nakutakia kila la kheri kwenye wiki nzuri inayoanza kesho.
Endelea kupitia hapa kila siku ili kujifunza mambo mazuri. Pia washirikishe ndugu, jamaa na marafiki zako ili nao wajifunze pia.
TUPO PAMOJA

Acha Kuifanya Hali Mbaya Kuwa Mbaya Zaidi.

Mara kwa mara kwenye maisha tunakutana na matatizo.
Baadhi ya matatizo haya yanaweza kuwa makubwa sana kiasi cha kutukatisha tamaa.
Lakini mara nyingi matatizo haya huanza kidogo na sisi wenyewe kuyafanya kuwa makubwa zaidi.
Moja ya njia tunayotumia kufanya hali mbaya kuwa mbaya zaidi ni kutumia hisia wakati unapokutana na hali mbaya.
Hisia hutufanya tuache kuangalia ukweli ni upi na kuishia kuona kwamba kwa nini sisi tunapata matatizo.
Acha sasa kutumia hisia pale unapokutana na matatizo. Tatizo lolote linapotokea, tulia na chambua tatizo hilo kwa kina kujua nini chanzo na unawezaje kulitatua.
Ila ukiingiza hisia utaona njia rahisi kwako ni kukata tamaa au hata kujiua.