Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, July 1, 2015

UKURASA WA 182; Urahisi Wa Kutengeneza Tabia Mbaya Na Ugumu Wa Kuishi Nazo.

Kuna jambo moja muhimu sana kwenye maisha ambalo unatakiwa kuwa unalijua. Na sio kulijua tu bali kulifanyia kazi kila siku maana kwa jambo hili moja ndio watu wanafanikiwa au wanashindwa.
Jambo hilo ni kwmaba, tabia mbaya ni rahisi sana kutengeneza ila ni ngumu sana kuishi nazo. Na kwa upande wa pili, tabia nzuri ni ngumu sana kutengeneza ila ni rahisi sana kuishi nazo. Hivyo ni wewe kuchagua kuwa tayari kufanya kipi ili uweze kuishije baadae.
Urahisi wa kutengeneza tabia mbaya.
Tabia mbaya ni rahisi sana kutengeneza, kwa mfano ulevi, ni rahisi sana kuwa mlevi, anza kunywa pombe kila siku na kunywa nyingi uwezavyo, hata hivyo unasikia raha, hivyo ni rahisi kutengeneza. Ila sasa maisha ya ulevi ni magumu sana, ni vigumu sana kuweza kufurahia maisha kama tayari wewe ni mlevi, utajikuta maisha yako yametawaliwa na ulevi na unajiona kama huwezi kutoka tena huko.
Tabia zote mbaya, iwe ni uvivu, wizi, uongo, kula hovyo zote ni rahisi sana kutekeleza. Ila kuishi nazo baada ya kuwa zimejijenga ni vigumu sana.
SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki Kimoja.
Ugumu wa kutengeneza tabia nzuri.
Kwa upande wa pili, tabia nzuri ni vigumu sana kuzitengeneza lakini ukishakuwa nazo ni rahisi sana kuishi nazo. Kwa mfano tabia ya kujiwekea akiba, ni vigumu sana mwanzoni, inabidi ujinyime inabidi uonekane huendi na wakati na wakati mwingine utahitaji kuzishinda tamaa zako. Ila unapokuwa na tabia hii ni rahisi na vizuri sana kuishi nayo kwa sababu unajua kuna akiba ambayo inaendelea kukua na hivyo kuvutiwa kuweka zaidi.
Unahitaji nguvu ya ziada ili kuweza kufikia mafanikio, ingekuwa rahisi kila mtu angekuwa nayo. Sio rahisi na ndio maana kuna wakati utaona kama unajitesa, endelea hivyo hivyo na mambo yatakuwa mazuri sana.
TAMKO LA LEO;
Najua nina machanguo mawili, nipate raha ya muda mfupi sasa halafu niteseke kwa muda mrefu au nipate shida ya muda mfupi sasa na kuishi kwa raha muda mrefu. Mimi nimechagua kuteseka kwa muda mfupi sasa ili niishi kwa raha muda mrefu ujao. Nitatengeneza tabia ambazo ni nzuri kwa sasa, ambazo ni ngumu kutengeneza lakini najua baadae nitafurahia kuishi nazo.
Tukutane kwenye ukurasa wa 183 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment