Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, July 7, 2015

UKURASA WA 188; Matatizo Yote Ya Mahusiano Huanzia Hapa.

Kama kuna kazi ngumu hapa duniani basi ni kuishi. Ndio maisha ni mazuri na ndio maisha ni matamu ila ni kazi kubwa sana kuweza kuyaishi.
Ni kazi kubwa kuyaishi kwa sababu huwezi kuishi maisha ya peke yako. Umezungukwa na watu wengi na watu hawa wana tabia tofauti tofauti. Watu wote hawafanani tabia.
Kuna wakati unafikiri kama watu wote wangekuwa kama fulani basi mambo yangekuwa mazuri sana. Saa nyingine unafikiria kama wateja wote wangekuwa kama mteja fulani basi biashara ingekuwa nzuri sana. Au wakati mwingine unafikiria kama bosi wako angekuwa na roho ya tofauti na aliyonayo sasa basi maisha yako ya kazi yangekuwa mazuri sana.
Lakini ukweli ndio huo kwamba watu hatufanani na pamoja na tofauti zote hizo bado unahitaji kushirikiana na watu wote hao.
SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.
Matatizo yote ya kwenye mahusiano, yawe ya kindugu, ya kibiashara, ya kikazi au hata ya kimapenzi yanaanzia pale mtu mmoja anapotaka kumbadilisha mwingine. Yaani ikishafikia hatua hii kwamba mtu mmoja anataka mwingine abadilike, ndio matatizo makubwa sana yanaibuka.
Unajua ni kwa nini? Kwa sababu mwanadamu atafanya kitu chochote kile kinachowezekana ili mradi tu asibadilike. Watu hawapendi kubadilishwa na wanapenda kuendelea kuwa vile walivyo. Tena kama ndio mtu mzima, ndio basi kabisa, atahakikisha anakataa kubadilika hata kama kufanya hivyo kunagharimu maisha yake.
Wakubali watu vile walivyo, au kama huwezi kuwakubali walivyo achana nao. Kama wataona wewe ni wa muhimu sana na hawawezi kukupoteza basi watabadilika wao wenyewe. Na mtu anapoamua yeye mwenyewe kubadilika inakuwa rahisi kwake kubadilika hata kwa kiasi kidogo. Ila kama wewe ndio unamlazimisha mtu abadilike, okoa nguvu zako.
TAMKO LA LEO;
Najua matatizo makubwa kwenye mahusiano ya watu huwa yana anza pale watu wanapojaribu kuwabadilisha wengine. Najua ya kwamba binadamu hawapendi kubadilishwa. Sitapoteza nguvu zangu kutaka kumbadilisha mtu. Nitamkubali mtu kama alivyo na kama siwezi nitaachana naye iwe ni mteja, bosi, ndugu au mwingine wa karibu. Muda wangu ni wa thamani sana siwezi kuupoteza kwa kufanya kazi ambayo haileti matunda.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment