Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, July 8, 2015

UKURASA WA 189; Matatizo Yote Ya Mahusiano Yanaanzia Hapa... Sehemu Ya Pili(2)

Jana nilikushirikisha sababu kubwa ya matatizo kwenye mahusiano yetu sisi na watu wengine. Na kama ukiweza kuondokana na chanzo kile basi utapunguza sehemu kubwa sana ya matatizo kwenye mahusiano yako iwe ya kikazi, kibiashara, kindugu au kimapenzi. Kama hukupata nafasi ya kusoma kile tulichojadili jana basi kisome hapa; Matatizo Yote Ya Mahusiano Huanzia Hapa.
Leo nataka tugusie kitu kingine kikubwa sana kinacholeta matatizo kwenye mahusiano yetu. Najua eneo la mahusiano ndio eneo gumu sana kuelewana na watu kwa sababu moja kubwa, inapokuja swala la mahusiano watu hawatumii akili kufikiri, bali wanatumia hisia kufikiri. Na pale hisia zinapojiongoza zenyewe bila akili basi hapo ni majanga. Ndio maana ni vigumu sana kuweza kumweleza mtu kuhusu mahusiano hasa ya mapenzi akakuelewa.
Sasa sababu nyingine kubwa ambayo inasababisha matatizo kwenye mahusiano ni watu kuvaa visanamu mwanzoni mwa mahusiano. Watu wanapokutana ili kujenga uhusiano, wengi wanadanganya, wanasema vitu ambavyo vitawafanya wakubalike au kupendwa na wale wanaotaka kuwa na mahusiano nao. Hii ni kwenye mahusiano yote, iwe ya kazi, biashara au hata mahusiano mengine ya karibu.
SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.
Mtu anadanganya kwenye usaili wa kazi ili aonekane ni bora na kupewa kazi. Labda hudanganyi vitu vikubwa, ni vitu vidogo vidogo tu kama kuahidi vitu ambavyo unajua kabisa huwezi kufanya kwa muda mrefu.
Au kwenye biashara unamdanganya mteja kwamba unaweza kufanya kitu fulani ili akubali kufanya biashara na wewe.
Kwenye mapenzi sasa, ndio mtu atadanganya vitu vingi sana, atabadili mpaka mfumo wa maisha, kuacha baadhi ya vitu na kadhalika.
Mambo yangekuwa rahisi sana kama kila mtu angeweza kuishi na hiki alichoahidi anaweza kufanya. Lakini kama tulivyoona jana, watu hawabadiliki, tena kwa haraka hivyo.
Kwa hiyo mtu atafanya kile alichosema kwa muda mfupi baada ya hapo anachoka na hivyo kurudia maisha yake ya zamani. Hapa ndio utasikia siku hizi fulani kabadilika. Hapana hajabadilika, amechoka kuvaa kile kisanamu na sasa ameanza kuonesha ukweli wake.
Kuwa makini usivae kisanamu wakati unataka kujenga mahusiano ambayo yatadumu. Kuwa mkweli, kama mtu hawezi kukukubali kwa ukweli wako hata ukimdanganya huo uhusiano hautadumu. Nasisitiza tena hii sio kwa mapenzi tu, bali kwenye mahusiano ya kazi, biashara na hata maisha ya kawaida. Kuwa mkweli na utawavutia wale wa kweli. Vaa kisanamu na utavutia visanamu vingine.
TAMKO LA LEO;
Najua kwamba kudanganya mwanzoni mwa mahusiano ni kujenga kifo cha mahusiano hayo. Hakuna uongo unaoweza kudumu kwa muda mrefu. Nitakuwa mkweli siku zote ili niweze kujenga mahusiano bora na yatakayoniletea mafanikio. Hata kama kuwa kwangu mkweli kutanikosesha baadhi ya mahusiano, najua kutanijengea mahusiano ambayo ni bora.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment