Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, July 9, 2015

UKURASA WA 190; Huwezi Au Hutaki? Kabla Hujaniambia Huwezi, Hakikisha Huponi.

Mpaka sasa umeshajifunza mambo mengi sana kuhusu mbinu za kuboresha kazi yako, biashara yako na hata maisha yako kwa ujumla. Lakini mbona bado huchukui hatua yoyote ili kuweza kunufaika na yale ambayo unajifunza?
Mpaka sasa unajua kabisa ya kwamba kwa kufanya kile ambacho kila mtu anafanya utaendelea kupata matokeo ambayo kila mtu anayapata na ambayo sio mazuri sana. Lakini mbona unaendelea kufanya hivyo?
SOMA; Maisha Ni Mchezo Na Sheria Za Kuushinda.
Mpaka sasa unajua kabisa kulalamika au kulaumu wengine hakutakupatia wewe chochote unachotaka, sana sana kutakufanya ujione kama yatima ambaye hana msaada wowote. Lakini bado unaendelea kulalamika na kulaumu, kwa nini?
Kwa sababu huwezi!! Hili ndio jibu ambalo unajiridhisha nalo. Kwamba siwezi kufanya tofauti, kila mtu ameshazoea vile nilivyo. Kwamba siwezi kuweka muda zaidi kwenye kujifunza, kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya. Kwamba siwezi kuacha kuangalia tv kila siku, nitapitwa na mambo mengi. Kwamba siwezi kuacha kukaa na jamaa zangu kila siku jioni tukipata moja moto na moja baridi ili nifuatilie zaidi biashara na kazi zangu.
Kama haya ndio majibu yako, kwanza wewe mwenyewe unayaamini kweli? Ni kweli kwamba huwezi kufanya mambo hayo ambayo yatabadili kabisa maisha yako? Vipi kama maisha yako ndio yangekuwa yanategemea hivyo ndio uweze kuishi. Kwa mfano unaambiwa kuchagua kuishi ila usiangalie tv au uangalie tv halafu unakufa, ungechagua nini?
Najua ungechagua kutokuangalia tv, safi sana, una maamuzi mazuri. Na ndio maana mimi siamini kwamba yale yote unayosema huwezi ni kwamba huwezi kweli, bali ni kwamba hutaki tu kufanya.
Kwa hiyo mambo yote unayosema kwamba huwezi, ukweli ni kwamba hutaki tu kufanya. Na kwa maana hii basi nakuomba kuanzia leo usiseme tena SIWEZI, sema SITAKI.
Siku nyingine kabla hujaniambia huwezi hakikisha kwamba ukifanya kitu hiko unakufa, vinginevyo ni sitaki.
TAMKO LA LEO;
Najua hakuna kitu kizuri na cha kubadili maisha yangu ambacho siwezi kufanya. Vingi ninavyoona siwezi kufanya ni kwamba sitaki tu kufanya. Kwa sababu kama maisha yangu yangekuwa yanategemea vitu hivyo ni lazima ningefanya. Hakuna kinachonishinda kufanya, na kuanzia sasa nitaacha kutumia sababu hii kwamba siwezi.
Tukutane kwenye ukurasa wa 191 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment