Kuna kauli nyingi sana kuhusu maisha. Mfano wa kauli hizo ni;
Maisha ni mapambano...
Maisha ni vita...
Maisha ni safari....
Na nyingine nyingi. Lakini leo nataka nikuambie kwamba katika kauli zote hizi kuhusu maisha, hakuna ambayo inayaelezea vizuri maisha. Na hapa tutajadili ile ambayo inayaelezea vizuri maisha yetu wanadamu.
Kauli inayoelezea maisha vizuri ni maisha ni mchezo. Ndio maisha ni mchezo na kama ilivyo michezo mingine kuna ambao wanashinda na kuna ambao wanashindwa. Na ili uweze kucheza vizuri mchezo wowote, kwanza kabisa lazima uzijue sheria za mchezo na uweze kuzitumia vizuri ili kushinda mchezo huo.
SOMA; BIASHARA LEO; Mtazamo Wa Kuvuna Na Mtazamo Wa Kujenga.
Maisha ni mchezo na katika mchezo huu kuna makundi mbalimbali ya watu. Kuna wale ambao ni wachezaji hasa ambao wapo uwanjani na wanacheza haswa, hawa ni wale ambao wanaishi maisha yao na wanayafurahia.
Pia kuna wale ambao ni washabiki, wanakaa nje ya uwanja na kuangalia mchezo. Hawa ni wale watu ambao hawana maisha yao wanayoishi, wao hufanya kile ambacho kila mtu anafanya. Watu hawa ni wazuri wa kukosoa wenzao, kama ambavyo mshabiki aliye nje ya uwanja anavyoweza kumkosoa mchezaji kwa urahisi.
Ili kushinda mchezo wowote kuna sheria muhimu unatakiwa kuzijua. Je unazijua sheria za kushinda huu mchezo wa maisha? Zipo wazi na hazina usumbufu. Kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa makala hizi mpaka sasa unazijua vizuri sheria hizi. Leo nataka niongeze moja muhimu;
Sheria ya kwanza na muhimu kabisa itakayokuwezesha kushinda kwenye mchezo huu wa maisha ni kuendelea kuwepo kwenye mchezo. Haijalishi ni kitu gani kimetokea, haijalishi ni changamoto gani unayopitia, ili uweze kushinda mchezo huu ni lazima uendelee kuwa uwanjani na uendelee kucheza. Hivyo ndivyo ilivyo kwenye maisha, haijalishi nini kimetokea, haijalishi ni changamoto gani unapitia, maisha lazima yaendelee.
Ongeza sheria nyingine kumi kwenye hii moja ambazo umeshajifunza mpaka sasa. Ukipenda nitumie kwa email, utakuwa umejiwekea msingi mzuri wa kuzifuata.
TAMKO LA LEO;Tukutane kwenye ukurasa wa 168 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Maisha ni mchezo na kama ilivyo michezo mingine yote, kuna sheria za mchezo huu. Sheria ya kwanza kabisa ya mchezo huu ni kwamba mchezo lazima uendelee hata kama kuna jambo baya kiasi gani limetokea. Maana ili uweze kushinda mchezo wowote ni lazima uwepo uwanjani na uweke juhudi na maarifa na nidhamu na uaminifu na......
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment