Kuna wakati
ambapo mambo yanaweza kuwa magumu sana kwako. Huu ni wakati ambapo unakuwa
umeweka malengo na mipango yako ila unashindwa kuyafikia. Unapanga kufanya kitu
fulani ili baadae upate majibu mazuri lakini hiyo pia haitokei.
Wakati kama
huu unaweza kujiona kama wewe una kisirani au huwezi kufikia kile unachotaka. Katika
wakati huu unaweza kuona wengine mambo yao yako vizuri ila ni wewe tu ambaye
mambo hayakwendi vizuri.
Leo nataka
nikuambie kwamba haijalishi unapitia magumu kiasi gani, haupo peke yako. Kuna watu
wengi sana wanaopitia magumu kama unayopitia wewe, lakini wanaendelea kuweka
juhudi kwa sababu wanajua huo sio mwisho. Kuna watu wengi ambao wanakazana
kuboresha maisha yao ila wanakutana na vikwazo vingi. Nao pia hawakati tamaa
kwa sababu wanajua hakuna kinachoshindikana.
Naomba nikusihi sana usikate tamaa hata pale mambo yanapokwenda tofauti na ulivyotegemea. Tafuta watu unaowaamini na ongea nao, kuna machache wanaweza kukuambia na ukajiona kumbe sio wewe mwenyewe umepotea kwenye dunia hii. Jua kwamba hata waliofikia mafanikio makubwa na unatamani kuwa kama wao, hawakufika pale kirahisi, walivuka vikwazo vingi ndio wakafika hatua ile. Unahitaji kuvuka vikwazo hivi pia.
TAMKO LA
LEO;
Pamoja na
changamoto nyingi ninazopitia kwenye kazi, biashara na hata maisha yangu kwa
ujumla, najua sipo peke yangu. Kuna watu wengi ambao wanapitia changamoto kama
mimi ila hawakati tamaa, wanaendelea kuweka juhudi. Najua hata wale ninaotamani
kufikia ngazi walizofikia walipitia nyakati ngumu pia. Nitaendelea kupambana na
kamwe sitokata tamaa.
Tukutane kwenye
ukurasa wa 157 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na
maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi
mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Pia washirikishe
wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia
watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kujifunza zaidi ili
kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment