Kwenye makala ya siku mbili zilizopita tuliona kwamba kila mtu anawinda fedha zako wewe. Kila mtu anayejaribu kukushawishi ununue kitu, kila anayekushawishi utoe fedha yako anaiwinda fedha yako. Kuna watu wengi sana wanaokuzunguka ambao wanawinda fedha yako, hivyo usipokuwa makini utashangaa umefanya kazi miaka mingi ila huoni kikubwa ulichobadili kwenye maisha yako.
Kama hukusoma makala iliyopita isome hapa; Kila Mtu Anawinda Kitu Hiki Muhimu Ulichonacho, Kuwa Makini.
Leo nataka nikushirikishe
njia nzuri itakayokuwezesha wewe kuwinda fedha zako mwenyewe. Njia hii
itakuwezesha kuona faida ya kipato ambacho unapata kwenye maisha yako kutokana
na kazi unazofanya.
Njia rahisi ya wewe kuwinda
kipato chako ni kujilipa wewe kwanza kabla hujafanya malipo mengine yoyote. Katika
fedha yoyote unayopata, hakikisha kuna kiasi fulani unaweka pembeni kabla
hujaanza kufanya matumizi. Kiasi hiki unaweza kuanzia na asilimia kumi ya
kipato chako.
Fedha yoyote unayoipata, iwe
ni faida kwenye biashara, mshahara wa kazi, umeokota au hata umepewa, usikubali
kuitumia yote. Igawe fedha hii kwenye mafungu kumi na chukua fungu moja weka
pembeni. Kama ni shilingi elfu kumi, weka elfu moja pembeni, kama ni laki moja
weka elfu kumi, kama ni milioni moja weka laki moja. Fedha hii unayoweka
pembeni ndio fedha uliyojilipa wewe mwenyewe na hutakiwi kuitumia kwenye
matumizi mengine yoyote.
Hii ni fedha yako ambayo
utaiwekeza ili iweze kukuzalishia zaidi baadaye. Kama utaweza kufanya hivi bila
kuchoka, baada ya muda utajikuta katika nafasi nzuri sana kifedha.
Jambo muhimu la kuzingatia ni
kwamba kuwa wa kwanza kuwinda fedha zako. Kabla hujafanya jambo lolote kwa
fedha yako, weka chako pembeni kwanza. Yaani usifanye matumizi halafu
itakayobaki ndio iwe yako ya kuwekeza. Bali wekeza kwanza na itakayobaki ndio
uipeleke kwenye matumizi.
TAMKO LA LEO;
Najua mimi ndio mtu wa kwanza
kuwinda fedha zangu kama ninataka kufikia uhuru wa kifedha. Kuanzia sasa, fedha
yoyote itakayopita kwenye mikono yangu, nitahakikisha asilimia 10 ya fedha hii
inabaki kuwa yangu. Sitakubali tena kuwa mpitishaji tu wa fedha, nataka na mimi
niwe sehemu ya fedha hizi. Nitakuwa mwindaji wa kwanza wa fedha zangu, kabla
sijawaruhusu wengine kufanya hivyo.
Tukutane kwenye ukurasa wa 135 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo
mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook
au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment