Kwa jinsi tulivyolelewa na kukuzwa, kushindwa ni kitu cha aibu sana, ni kitu kinachostahili adhabu kubwa na kama utashindwa basi wewe ni mtu ambaye hufai. Si ndio tulivyofundishwa shuleni? Na ndio maana tulipewa adhabu kali pale ambapo tulishindwa kwenye kazi au mtihani.
Kinyume na ilivyo kwenye elimu na hata kwenye malezi uliyopewa, kwenye maisha ya kawaida kushindwa ni kitu kizuri sana. Kushindwa ni muhimu kwa sababu unajifunza mambo mengi kuliko unavyoshinda. Japo wengi hawaamini hili na hawataki hata kusikia.
Kwa woga wetu wa kushindwa, wengi wetu wamekuwa wakiogopa hata kuweka malengo makubwa kwa kuogopa kushindwa. Mtu anaona kama aliweka malengo makubwa na akashindwa kuyafikia basi ni sawa na kujidhalilisha. Kwa sababu hiyo anaweka malengo madogo ambayo yapo ndani ya uwezo wake na anayafikia vizuri.
SOMA; Hii ndio faida ya kushindwa.
Sasa kuweka malengo ambayo yako ndani ya uwezo wako na ukayafikia vizuri, unafikiri ni kitu gani kikubwa umejifuza? Hakuna, yaani umeendelea kuwa vile ulivyokuwa na huwezi kufikia mafanikio makubwa.
Lakini unapoweka malengo makubwa, malengo ambayo hata wewe mwenyewe yanakuogopesha, haya ndio malengo ambayo yatakusukuma ufanye zaidi na hata kama hutayafikia, utamaliza ukiwa mbali kuliko ungeweka malengo madogo.
Hivyo kuanzia leo na kwa muda wote uliobakia, malengo yote uliyoweka mwanzo yazidishe mara kumi na anza kuangalia ni njia gani zitakufikisha pale. Ndio weka mara kumi halafu umiza kichwa chako na weka juhudi mpaka tone la mwisho. Huenda hutafikia mara 10 lakini utafikia mara 5 au hata mara 3 ambayo ni bora zaidi ya kama ungeendelea na lengo lako la mwanzo.
TAMKO LA LEO;Tukutane kwenye ukurasa wa 176 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Najua naogopa sana kushindwa, najua naona kushindwa ni kama aibu kwangu. Lakini nimeshajua kwamba kushindwa ni sehemu muhimu sana kwenye maisha ya kila siku. Kuanzia sasa nitaweka malengo makubwa na ambayo yatanisukuma kila siku ili kufanya zaidi ya ninavyofanya sasa. Kwa kuweka malengo makubwa hata kama sitayafikia nitajifunza na kuwa mbali zaidi kuliko nikiweka malengo madogo na ambayo naweza kuyafikia.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment