Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, June 25, 2015

UKURASA WA 176; Hiki Ni Kipimo Kibovu Sana Cha Kupima Mafanikio Yako.

Kuna watu walikaa chini wakaamua kwamba kuwe na mtihani mmoja na wanafunzi wote waufanye, atakayepata maksi nyingi ndio amefaulu, atakayepata chache amefeli.
Kuna watu pia wamekaa wakakubaliana kwamba ukiwa na magari ya kifahari, ukawa na nyumba ya kifahari na fedha isipokuwa tatizo kwako basi wewe umefanikiwa.
Vyote hivi vinaweza kuwa vipimo kwa sababu vitakusukuma na wewe uweze kufika mbali zaidi ila sio vipimo sahihi kwa mafanikio yako. Hivi ni vipimo vibovu sana kwako kujipima kama umefikia mafanikio au la.
Hakuna kipimo kimoja kinachoweza kupima mafanikio ya watu wote kwa kigezo kimoja, ndio maana mara zote nimekuwa nakusisitizia sana usijilinganishe na wengine. Ni vizuri kujua wengine wanafanya nini, ila usijione umeshinda au umeshindwa kwa sababu ya kile unachofanya unavyokilinganisha na wengine wanavyofanya.
Kwa kifupi ni kwamba usipime mafanikio yako kwa vigezo ambavyo vimewekwa na watu wengine. Utakuwa hujitendei haki na kinaweza kuwa kikwazo kikubwa sana kwako kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Sasa ujipime na nini?
1. Jipimie kwa malengo makubwa uliyojiwekea? Je umeyafikia? Na kama hujayafikia ni kwa nini na umejifunza nini? Hakikisha malengo hayo ni makubwa; soma hapa kujua umuhimu wa malengo makubwa; Ni Bora Kuweka Malengo Makubwa Na Kushindwa Kuliko Kuweka Malengo Madogo Na Kushinda.
2. Jipime kwa juhudi unazoweka, je ni juhudi za kutosha? Je zinaleta matunda unayotarajia?
3. Jipime kwa ulivyokuwa jana na utakavyokuwa leo. je leo uko bora zaidi ya ulivyokuwa jana? Je kadiri siku zinavyokwenda unazidi kuwa bora au unazidi kuwa hovyo?
4. Jipime kwa maisha ya wengine uliyogusa. Je ni kwa kiasi gani watu wengine wamenufaika kwa kile ambacho unafanya? Je wataendelea kunufaika na kile unachofanya? Je watakukumbuka hata usipokuwepo?
Hivi ni baadhi ya vigezo sahihi kwako kujipima kama kweli umefikia mafanikio au la. Vigezo vinavyotengenezwa na wengine ni sumu kwako, usijaribu kuvitumia.
TAMKO LA LEO;
Nimekuwa napima mafanikio yangu kwa vigezo ambavyo vimewekwa na watu wengine. Njia hii imekuwa inaniumiza na kunirudisha nyuma. Kuanzia sasa nitapima mafanikio yangu kwa vigezo vyangu mwenyewe na nitahakikisha navifikia na kuweka vikubwa zaidi ili kila siku niwe bora zaidi ya siku iliyopita.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment