Hofu ni moja
ya vitu ambavyo vinawazuia watu wengi kuweza kupiga hatua kwenye maisha yao. Hofu
imewafanya watu wengi kushindwa kuzichangamkia fursa zinazowazunguka na hivyo
kushindwa kufikia mafanikio kwenye maisha.
Moja ya hofu
kubwa zinazowazuia wengi kupata maendeleo ni hofu ya kupoteza. Mtu akishakuwa
na kitu, hufanya kila lililo ndani ya uwezo wake ili kulinda kitu hiko. Hakuna anayependa
kupoteza kitu ambacho amekifanyia kazi kwa muda mrefu.
Lakini pia
kuhofia kupoteza kitu ulichonacho maana yake utashindwa kuchukua hatua kwenye
fursa mbalimbali zitakazojitokeza. Kama tunavyojua kwenye maisha, kitu chochote
kizuri huwa kinakuja na hatari zake(risk). Hivyo ili upate faida ni lazima
ufanye kitu ambacho kinaweza kuwa hatari kwako. Unakuwa na uwezekano mkubwa wa
kupoteza kama ilivyo kwenye kupata.
Unapojikuta
kwenye hali ya hofu kama hii, pia kiasi ambacho unaweza kupoteza na pia pima
kile ambacho utakipata kama ukichukua hatua. Pia pima ni kitu gani unajifunza
kama utachukua hatua na ukapoteza. Pia angalia njia nyingine unazoweza kutumia
kupunguza hatari hiyo. Baada ya hapo chukua hatua mara moja.
Watu wengi
watakuambia chukua risk, fanya na utajifunza, ila usiingie kichwa kichwa,
hakikisha hata kama utapoteza basi kuna
somo utajifunza.
TAMKO LA LEO;Najua hofu imekuwa inanizuia kufikia malengo yangu kwenye maisha. Hofu ya kupoteza imekuwa inanizuia mimi kuzichangamkia fursa zinazojitokeza. Kuanzia sasa nitakuwa nafanyia kazi fursa inayojitokeza kwa kuhakikisha hata kama ninapoteza kuna somo kubwa ninalojifunza.
Tukutane kwenye
ukurasa wa 160 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na
maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi
mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Pia washirikishe
wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia
watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kujifunza zaidi ili
kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment