Lengo la kila makala ninayoandika, lengo la kila ujumbe ninaoutoa wka njia mbali mbali iwe ni maongezi au hata video(angalia na jiunge na AMKA TV) ni kukupa wewe maarifa na mbinu za kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Kwa kuwa hiki ndio unachotaka kwenye maisha yako, au sio?
Leo nataka nikushirikishe baadhi ya vitu ambavyo usikubali kabisa kujishikiza navyo kwenye maisha. Kwa kujishikiza na vitu hivi unajiandaa kukatishwa tamaa na kuyafanya maisha yako kuwa magumu sana.
Tumewahi kujadili hapa kuhusiana na vitu tunavyokutana navyo kwenye maisha. Na tukasema kila kitu ulichanacho au unachokutana nacho kwenye maisha kinaingia katika moja ya makundi haya mawili. Kundi la kwanza ni vitu unavyoweza kuviathiri au kuvidhibiti na kundi la pili ni vitu ambavyo huwezi kuviathiri au kuvidhibiti.
Sasa leo nataka tujadili vitu ambavyo huwezi kuviathiri au kuvithibiti. Vitu unavyoweza kuviathiri tulishavijadili kwenye makala hii; Kitu Pekee Unachoweza Kukidhibiti Kwenye Maisha Yako.
Kwenye maisha yako usijishike na vitu ambavyo huwezi kuvidhibiti, utajitengenezea nafasi kubwa ya kuumia moyo na kukatishwa tamaa. Huwezi kudhibiti ni kwa muda gani familia yako na marafiki zako wataishi. Huwezi kudhibiti ni kwamba utapandishwa cheo kazini au la. Huwezi kudhibiti kwamba kila biashara utakayofanya lazima ufanikiwe. Huwezi kudhibiti kama mwenza au mchuma uliyenaye mtakuwa pamoja mpaka kifo kiwatenganishe.
Hivi ni baadhi ya vitu vilivyopo nje ya uwezo wako wa udhibiti, japo unaweza kutengeneza mazingira mazuri na kuwa na vitu hivyo. Lengo la kujadili haya ni wewe kutouweka maisha yako yote katika vitu ambavyo huwezi kuvidhibiti. Kujua kwamba lolote linaweza kutokea ambalo lipo nje ya uwezo wako na likavuruga kila ambacho ulikuwa unaamini.
Hivyo furahia vitu kama vilivyo ila jua vinaweza kubadilika muda wowote bila ya wewe kutaarifiwa.
TAMKO LA LEO;Tukutane kwenye ukurasa wa 167 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Najua kuna vitu vingi kwenye maisha siwezi kuvidhibiti. Kuanzia sasa sitoshikilia maisha yangu kwenye vitu hivi. Nitavifurahia wakati ninavyo na nitafanya juhudi zilizopo ndani ya uwezo wangu kuvikuza viwepo, ila pale vitakapoondoka kwa sababu ambazo siwezi kuzizuia nitajua ni sehemu ya maisha na sitokata tamaa na maisha yangu.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment