Mara nyingi huwa tunafikiri wkamba tunaweza kuwadhibiti watu, kudhibiti hali zinazotokea, kudhibiti fedha na mambo mengine mengi. Ila tunapojaribu kudhibiti vizu hivi tunashindwa vibaya sana. Kwa kushindwa huku tunaweza kujiona kama hatufai au hatuwezi kuendesha maisha yetu vizuri.
Leo nataka nikuambie kwamba kushindwa kudhibiti vitu hivyo unavyotaka kudhibiti hakumaanishi kwamba maisha yako hayafai. Ila ni kwamba hujajua ni vitu gani unavyoweza kudhibiti na vitu gani huwezi kudhibiti. Kuna kitu kimoja tu ambacho unaweza kukidhibiti kwenye dunia hii na kwenye maisha yako. Kwa mudhibiti kitu hiki kimoja, vitu vingine vyote vinakwenda sawa, hata kama utakuwa hujavidhibiti.
SOMA; Hii Ndio Siri Ya Kupata Marafiki Bora Watakaokuwezesha Kufikia Malengo Yako.
Kitu pekee unachoweza kudhibiti kwenye dunia hii na kwenye maisha yako ni mawazo yako. Unaweza kuchagua ni mawazo gani yaingie kwenye akili yako na ni mawazo gani unayoweza kuyafanyia kazi. Huu ni uhuru mkubwa sana kwako na kama utawez akuutumia vizuri basi utaweza kukupatia chochote ambacho unataka. Kama ambavyo unajua, chochote kinachotokea kwenye maisha yako kinatokana na mawazo yako. Hivyo ukiweza kudhibiti mawazo yako, utaweza kudhibiti ni kitu gani kinatokea kwneye maisha yako. Jinsi unavyoyachukulia maisha ndivyo yanavyotokea. Na jinsi unavyowafikiria watu ndivyo wanavyokutendea.
Hivyo kama unataka kudhibiti maisha yako, kama unataka kuboresha maisha yako, anza kwa kudhibiti na kuboresha mawazo yako. Kuwa na mawazo ya yale mambo unayotaka, kuwa na mawazo chanya na jione wewe ni wa tofauti na una uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko kwenye maisha yako na ya wanaokuzunguka. Kama unataka mabadiliko, anza wewe kubadilika. Kwa kufanya hivi utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako, sio kwa sababu umewadhibiti au kuwabadili watu, ila kwa kuwa umeweza kudhibiti mawazo yako.
SOMA; Hatua Saba (7) Za Kuweka Malengo Na Kuweza Kutimiza Ndoto Zako.
TAMKO LA LEO;
Najua kitu pekee ninachoweza kukidhibiti kwenye maisha yangu ni mawazo yangu. Mimi ndio ninayeweza kuamua nifikirie kitu gani na kitu gani nikipe kipaumbele. Kwa kuweza kudhibiti maisha yangu nitaweza kudhibiti sehemu kubwa ya maisha yangu. Sitakubali mawazo hasi na ya hovyo yatawale akili yangu. Nitaweka mawazo chanya na ya mabadiliko katika akili yangu na nitayafanyia kazi.
Tukutane kwenye ukurasa wa 146 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment