Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, May 7, 2015

UKURASA WA 127; Kinachokufanya Ukwame, Na Uwe Na Maisha Magumu.

Sehemu kubwa ya maisha yako kuwa magumu inasababishwa na wewe mwenyewe. Binadamu tumekuwa na tabia ya kufanya maisha yetu kuw amagumu kadiri siku zinavyozidi kwenda na kadiri tunavyofanikiwa.

Chanzo kikuu cha maisha ya watu kuwa magumu ni kuishi maisha ya maigizo. Hakuna kitu kinachoweza kumuuziza mtu kama kuishi maisha ya maigizo. Maisha ya maigizo ni yale maisha ambapo unataka uonekane ni mtu wa aina fulani kumbe siyo. Unaweza kuwadanganya watu kwa maigizo yako ila kamwe huwezi kujidanganya wewe mwenyewe na mara zote utakuwa na mgogoro wa nafsi.

SOMA; Dalili Kwamba Unaweza Kufikia Mafanikio Makubwa.

Mgogoro huu utakupelekea kujiona wewe huwezi au umeshashindwa. Na ili uweze kuendelea na maigizo yako utajikuta unajiingiza kwenye matatizo makubwa sana. Unaweza kujikuta umeingia kwenye matatizo makubwa sana kifedha kwa sababu tu umefanya jambo ambalo unataka wengine wakuone na wewe upo. Jambo hilo linaweza lisiwe muhimu sana kwako, lakini kwa kuwa maisha yako ni ya maigizo unalazimika kulifanya.

Na mbaya zaidi kwenye maisha ya maigizo, kile ambacho ulikuwa unafikiri utakipata kwa kuigiza, unakikosa kabisa. Kwa hiyo juhudi zako zote zinakuwa zimeishia hewani na unakuwa umejidhulumu maisha yako mwenyewe.

SOMA; Kama Mteja Anaweza Kununua Kwa Mtu Yeyote, Kwa Nini Anunue Kwako?

TAMKO LA LEO;

Najua sehemu kubwa ya ugumu wa maisha yangu ninausababisha mwenyewe, kwa kufanya mambo ambayo yapo nje ya uwezo wangu ili tu nionekane kwa wengine. Maisha haya ya kuigiza sio mazuri kwangu, kwani nitakuwa najidanganya na hata kile nilichokuwa nategemea kupata nitakikosa. Nitaishi maisha ya ukweli kwangu bila ya kujali wengine wananichukuliaje. Kila mtu ana matatizo yake kwenye maisha, sitaki kujiongezea mengi zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 128 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment