Kuna vitu vingi sana ambavyo vinatokea hapo ulipo.
Kuna fursa nyingi sana ambazo zimekuzunguka.
Kuna mambo mazuri sana kwenye maisha yako na hata kazi/biashara yako ambayo ukiweza kuyatumia vizuri yatakuletea mafanikio makubwa.
SOMA; Kitu Pekee Kinachoweza Kuiharibu Siku Yako Na Jinsi Unavyoweza Kuepuka…
Lakini wewe huyaoni. Huyaoni sio kwa sababu huangalii ila kwa sababu hutaki kuona. Katika hali moja watu wawili wanaweza kuwa wanaangalia na mmoja akaona vitu vizuri wakati mwingine anaona vitu vibaya.
Kuona kunaanza na akili yako mwenyewe. Kumbuka huwezi kuona kile ambacho akili yako haikijui. Ukimuona mjusi unajua huyu ni mjusi kwa sababu akili yako inajua mjusi ni nini.
Kuna fursa nyingi ambazo zinakuzunguka hapo ulipo lakini huzioni kwa sababu hujataka kuziona. Na kama unataka kuziona basi jua ni nini kipo, ni nini unataka halafu anza kuangalia. Utaona.
Umewahi kuona kitu hiki, labda mtu anakuambia eneo unalokaa lina magari mengi mekundu. Huenda ulikuwa hujawahi kuliweka maanani hili, lakini baada ya kuambiwa hivyo utaanza kuona magari mekundu kila unapopita. Sio kwamba magari haya yameanz akuongezeka sasa, ila umeamua kuyaona na sasa unayaona mengi sana.
SOMA; Kitu Hiki Kimoja Ni Muhimu Kuliko Kiwango Cha Fedha Unachotaka.
Ili kuziona fursa na uweze kuzitumia, jua kwanza ni fursa gani unazotaka na jua pia kwamba zinapatikana. Na utaanza kuziona nyingi kuliko ilivyokuwa awali.
TAMKO LA LEO;
Najua sioni sio kwa sababu siangalii ila kwa sababu sijaamua kuona. Kama nataka kuona fursa, ni lazima nijue ni fursa zipi nataka na zipi zinapatikana. Nitaanza kuona fursa hizi kwenye kila kitu ambacho nitakigusa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 25kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment