Moja ya
vitu vizuri nilivyojifunza kwenye maisha ni kwamba, watu huwa wanayafanya
maisha yao kuwa magumu wao wenyewe. Yaani kama unaona maisha yako ni magumu,
basi wewe mwenyewe umechangia sehemu kubwa sana ya ugumu huo. Unaweza kukataa
na kusingizia kila kitu unachoweza, serikali ambayo haitoi ajira, uchumi ambao
ni mgumu, wazazi ambao hawakukujali, ndugu ambao hawataki kukusaidia na mengine
mengi unayoweza kufikiria.
Kuna sababu moja kubwa sana
inayokufanya unaendelea kukwama kila siku kwenye maisha yako na hii inafanya
maisha yawe magumu kwako. Sababu hii ni kwamba unajaribu kuwa mtu ambaye siye
ulivyo. Umekuwa unaiga mambo ya wengine na kutaka maisha yako yawe kama ya watu
wengine. Kwa kukazana kufanya hivi unasahau lengo lako muhimu kwenye maisha na
hivyo kujikuta unakimbiza kila lengo linalotokea mbele yako. Ukiona mtu kanunua
kitu na wewe unataka ununue, sio kwa sababu unahitaji, bali kwa sababu na wewe
unataka usibaki nyuma.
Wakati mwingine unajikuta unalazimika
kuishi maisha ambayo sio unayopenda kwa sababu tu jamii nzima inaishi hivyo. Imekuwa
ni kawaida kwa jamii kutupangia ni jinsi gani tutakavyoishi, ni kazi au
biashara gani tunaweza kufanya na hata maisha tunayoishi. Kwa kutaka kwenda na
jamii kwenye hali hii ndio kunasababisha maisha yanakuwa magumu sana kwa sababu
hufanyi kile ambacho kinatoka moyoni mwako na hivyo unakosa furaha.
SOMA; Wajue Watu Hawa Wanaokazana Kukurudisha Nyuma Na Jinsi Ya Kuwashinda.
Amua sasa kushika hatamu ya
maisha yako, amua kufanya kazi au biashara unayopenda, amua kuishi maisha
ambayo utayafurahia. Tuna muda mfupi sana wa kuwepo hapa duniani, tafadhali
usiupoteze kwa kuishi maisha ambayo huyafurahii. Ishi maisha ambayo yataleta
tofauti kwako na kwa wale wanaokuzunguka, na hata ukiondoka utaacha alama.
TAMKO LA LEO;Najua sehemu kubwa ya ugumu wa maisha yangu nasababisha mwenyewe, kwa kujaribu kuishi maisha ambayo sio yangu, kwa kutaka kufanya kile ambacho kila mtu anafanya na kwa kulazimika kuishi kama vile ambavyo jamii inataka niishi. Kuanzia sasa nakataa maisha ya aina hii, na nitaishi yale maisha ambayo nayapenda na yataleta tofauti kwangu na kwa wanaonizunguka.
Tukutane kwenye ukurasa wa 151 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na
maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza
hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA
MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment