Leo nakupa siri kubwa sana ambayo huenda sijawahi kukupa japo nimekuwa nakuandikia kila siku. Siri hii imeniwezesha kufanya mambo mengi ambayo awali nilikuwa naona siwezi kuyafanya. Hata wewe kuna mambo mengi sana ambayo unaona huwezi kuyafanya ila sio kwmaba huwezi kweli, bali kuna kitu unachokilinda na kitu hiko kinakuzua wewe kuweza kuchukua hatua.
Je ni kitu gani hiki ambacho unakilinda na kimekuwa adui kwako? Kitu hiki ni hadithi ya maisha yako. Kama nilivyowahi kuandika kwenye makala moja iliyopita, hakuna kitu chenye nguvu kama hadithi ya maisha yako unayojiambia kila siku. Hizi ni zile fikra ambazo zimejaa kwneye akili yako, hivi ndivyo ambavyo unajiona na hivyo matendo yako yote ni lazima yaendane na hadithi hii.
SOMA; Kanuni 6 Za Kuweza Kukusaidia Kuishi Wewe Kama Wewe Katika Maisha Yako.
Kwanzia mwaka huu umeanza kila siku, yaani kila siku nimekuw anakuandikia makala hapa kwenye KURASA 365 ZA MWAKA 2015, sijakosa hata siku moja na makala zote naziandika wakati huo huo na kuzituma, sio kwamba naandika nyingi kwa wakati mmoja na kuziweka tu hewani(japo ningeweza kufanya hivyo). Sasa unajua ni mara ngapi nimekuwa napata sababu zinazonizuia nisiandike kwenye baadhi ya siku, mara nyingi mno. Kuna siku nimewahi kuona wacha leo ipite tu, sio mbaya sana. Lakini sikuweza kuruhusu hilo. Hii ni kwa sababu naishi nalinda hadithi ya maisha yangu. Nilishakuahidi kwmaba kila siku nitakuandikia makala moja kupitia mtandao huu Makirita AMani, haijalishi ni siku ya aina gani, haijalishi ni sikukuu gani, nimeshaweka ahadi yangu kwako. Na kwa sababu naheshimu sana wewe kuniamini, lazima nitimize ahadi yangu, kwa vyovyote vile. Ungana nami facebook kwa kubonyeza Coach Makirita Amani na tutapeana mbinu nyingi.
Na wewe pia unaishi hivi kila siku. Unajifunza kitu kizuri sana ambacho kinaweza kubadili maisha yako, unajifunz ambinu nzuri ya kuongeza juhudi kwenye kazi yako au biashara yako, lakini kabla hujaitekeleza unajikumbusha hadithi ya maisha yako, lakini mimi ni mvivu, kila mtu anajua mimi ni mvivu. Habari inaishia hapo.
SOMA; Kumbuka Sio Lazima Ufanye Kitu Hiki…
Unaona kabisa mabadiliko ni muhimu kwneye maisha yako. Unahitaji kubadili tabia zako, inabidi uache ulevi na upate muda w akufanya mambo ambayo ni muhimu kwako. Lakini kabla hujatekeleza mipango yako hiyo unajikumbusha hadithi ya maisha yako, lakini mimi ni mlevi, kila mtu anajua mimi ni mlevi. Unaendelea kulidna hadithi yako hii.
Leo nataka nikuambie kwamba hujafunga ndoa ya milele na hadithi yoyote unayojiambia sasa, haijalishi inajichukuliaje sasa, au wengine wanakuchukuliaje, bado unayonafasi ya kubadilika katika kipindi chochote cha maisha yako. Kama umeamua sasa imetosha na inabidi nibadilike, usikimbilie kuchukua hatua, utapoteza muda wako bure. Anza kwanz akutengeneza hadithi mpya ya maisha yako. Jione wewe ni mtu uliyabadilika, jione ni mtu wa kutimiza ahadi zako na waahidi watu usiotaka kuwaangusha ni nini unakwenda kufanya. Halafu anza kufanyia kazi mipango yako.
SOMA; Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani
TAMKO LA LEO;
Najua hadithi ya zamani ya maisha yangu ndio inanizuia mimi kufikia mafanikio. Kuanzia sasa nabadilisha hadithi ile na kwa sasa mimi ni mtu ambaye ni mchapakazi, mtu anayejituma, mtu anayeweka juhudi na maarifa kwenye kila anachofanya ili kiwe bora zaidi. Hii ndio picha ambayo kila anayeniangalia nataka aione. Nitailinda hadithi hii ili nifikie mafanikio makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 136 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment