Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, May 2, 2015

UKURASA WA 122; Dalili Kwamba Unaweza Kufikia Mafanikio Makubwa.

Moja ya vitu vinavyoweza kutuonesha kama kitu kinawezekana au hakiwezekani ni utafiti. Ndio maana kabla ya mtu kuingia kwenye biashara anahitaji kufanya utafiti ili kujua kama kuna wateja ambao wanahitaji huduma au bidhaa anazotoa. Hata kwenye sayansi, kabla kitu hakijapitishwa lazima ufanyike utafiti. Kabla dawa yoyote haijapitishwa kwa matumizi ya binadamu ni lazima ifanyiwe tafiti mbalimbali na ikionesha majibu mazuri ndio inapitishwa.

SOMA; Siri Hii Itakusaidia Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi - 3

Sasa leo nataka nikuoneshe kwamba wewe hapo unawez akufikia mafanikio makubwa sana kwenye maisha kwa kuanzia hapo ulipo tu, bila ya kuangalia umekosa nini. Yaani hata kama huna mtaji mkubwa, hata kama huna elimu ya kutosha, bado unaweza kufikia mafanikio makuwba sana. Nina uhakika huo na hapa nitakuambia kwa nini.

Uhakika ni kwmaba kuwepo kwa watu ambao tayari wamefanikiwa, kunaonesha kwamba mafanikio yanawezekana. Kuwepo kwa watu ambao wameanzia chini kabisa lakini wakaweza kutoboza hii inatuonesha kwamba kuna uwezekano wa watu waliopo chini kutoboza. Kuwepo wka watu ambao hawana elimu kubwa ila wameweza kufikia mafanikio makubwa kunaonesha kwamba ukosefu wa elimu sio kikwazo cha kufikia mafanikio. Kuwepo kwa watu ambaow alianza biashara kw akiwango cha chini sana lakini sasa wanamiliki biashara kubwa kunaonesha kwamba ukosefu wa mtaji sio kikwazo.

SOMA; Jambo Muhimu La Kila Mfanyabiashara Kufanya Kila Siku.

Sasa unafanyaje ili na wewe uweze kufikia mafanikio ambayo hao wengine wamefikia? Rahisi, wajue watu hao waliofanikiwa, jifunze ni njia gani walizotumia na wewe anza kutumia njia hizo. Sio kuiga bali kutumia njia ambayo imeonesha majibu kwa wengine.

Na mengi wanayofanya watu hawa sote tunayajua, kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kuwa mwaminifu, kuwa mvumilivu, kuwa mbunifu, kujali mambo yako, kuacha kulalamika na mengine mengi. Mengi unayajua sema tu hutaki kuyafanyia kazi. Anza kuyafanyia kazi sasa na maisha yako hayatabaki yalivyo sasa.

SOMA; Hiki Ndicho Kitu Unachotakiwa Kuwa Makini Nacho Sana Ili Kufanikiwa.

TAMKO LA LEO;

Kuwepo kwa watu ambao wamefikia mafanikio makubwa licha ya kuanzia chini, kunaonesha kwamba hata mimi naweza kufika mbali zaidi ya nilipofika sasa. Nitaendelea kujifunza na kutumia yale ninayojifunza ili kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 123 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment