Kuna njia mbili za kuitazama dunia, ambazo unaweza kuchagua moja kati ya hizo mbili.
Njia ya kwanza ni kuitazama dunia kama ina wingi wa kila kitu. Kuiona dunia ina wingi wa fursa za kukupatia wewe kipato na mafanikio. Kuiona dunia kama ina wingi wa watu wema na unaoweza kushirikiana nao kuboresha maisha yako. Kuiona dunia kama ina wingi wa fedha, wingi wa watu wenye mafanikio na waliotayari kuwasaidia wengine.
SOMA; Tofauti ya mtazamo Kati ya Mtu wa Hali ya kati na Mtu wa hali Juu.
Njia ya pili ni kuitazama dunia kama ina uhaba wa kila kitu. Kuiona dunia kama ina uhaba wa fursa za kukupatia wewe kipato na mafanikio. Kuiona dunia kama ina uhaba wa watu wema na kukosa ushirikiano mzuri kutoka kwa wengine. Kuiona dunia kama ina uhaba wa fedha na uhaba wa watu wenye mafanikio na uhaba wa watu waliotayari kuwasaidia wengine.
Kuna tofauti moja kubwa kati ya mitazamo hiyo miwili. Wenye mtazamo wa kwanza wanakuwa na maisha mazuri, yenye furaha na mafanikio makubwa. Wenye mtizamo wa pili wanakuwa na maisha ya hofu, ya uchoyo na yasiyokuwa na mafanikio.
SOMA; Huoni Kwa Sababu Hutaki Kuona.
Ona dunia yenye wingi na wingi utakuja kwenye maisha yako. Ona dunia yenye uhaba na uhaba utatawala maisha yako.
TAMKO LA LEO;
Nikiwa na mtazamo wa wingi nitaona vingi kwenye dunia hii na nitafikia mafanikio. Nikiwa na mtazamo wa uhaba nitakosa vingi na nitashindwa kufikia mafanikio. Kuanzia sasa nitaiona dunia yenye wingi.
Tukutane kwenye ukurasa wa 130 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment