Njia rahis ya wewe kutengeneza matatizo makubwa sana kwenye maisha yako ni kuepuka mambo, kukataa majukumu na kupingana na ukweli. Hiki ni kitu ambacho umekuwa unafanya kila mara kabla hujaingia kwenye matatizo makubwa.
Kama unakataa, kaa chini leo na angalia kwenye kila tatizo kubwa ulilowahi kukutana nalo kwneye maisha kama utakosa vitu hivyo vitatu. Lazima katika wakati wowote kabla ya tatizo hilo uliepuka kufanya jambo ambalo ni muhimu, au ulikwepa kutimiza majukumu yako kwa usahihi na kwa wakati au ulipingana na ukweli.
SOMA; Kwanini ni Muhimu kuwekeza kwa Muda Mrefu.
Haihitaji uwezo wa kipekee au elimu kubwa kuliona hili, lakini tunachagua kutokuliona, unajua kwa nini? Kwa sababu tatizo lolote linapotokea hatukosi mtu wa kumlaumu au kumlalamikia. Na tukishafanya hivi tunasahau nafasi yetu katika kusababisha tatizo hilo.
Kabla mtu hajaumwa na kuwa hoi kitandani, anakuwa na dalili ndogo ndogo za ugonjwa. Kwanza kabla hata ya dalili hizo ndogo ndogo, ataacha kuijali afya yake, kula vyakula visivyo vya afya, kukaa kwenye mazingira hatarishi kiafya. Baadae dalili ndogo ndogo zinaanza, bado hakubali kwamba atakuwa mgonjwa, anatumia dawa za maumivu au chochote kitakachomsukuma kwa siku chache. Baadae mweili unachoka na kushindwa kuendele akupambana na ugonjwa na ndio mtu anakuwa mahututi. Anapofika hospitalini katika hali hii na ikatoke ahakupata huduma nzuri lawama zake zote atapeleka kwa watoa huduma, hivyo yeye hatakuwa na mchango wowote kwenye tatizo lake.
SOMA; Anza Na Tatizo Ulilonalo, Halafu Biashara.
Mtu anaanza biashara na anakuwa na kipango muzuri, biashara inafanya vizuri na yeye anajisahau, anaanza kula raha au kuw ana matumizi ya fedha yasiyo mazuri, biashara inaanza kujiendesha wka hasara, lakini bado haoni hilo. Pale hali inapokuwa mbaya kabisa ndio anastuka kwamba biashara inakufa, anaanza kutafuta nani wa kumlaumu.Hapa ndio utasikia kuna chuma ulete, mara mtaa sio mzuri wk abiashara, mara hii biahsara haifai, mara watu wameniondoa kwa ushirikina. Na mengine mengi.
Sasa jua matatizo yote unayokutana nayo kwenye maisha hayaanzi ghafla, yanakuwa na viashiria vyake. Na pale wewe unapokosa umakini, au kukwepa majukumu au kukataa ukweli ndio unazidisha tatizo na kuathirika zaidi.
SOMA; Jinsi Ya Kutengeneza Fedha Kwenye Mtandao Kwa Kutumia Blog
TAMKO LA LEO;
Najua mimi mwenyewe nimekuwa nikitengeneza na kukuza matatizo kwenye maisha yangu. Nimekuwa nikiepuka mambo, nimekuwa nikikwepa majukumu yangu na pia nimekuwa nikipingana na ukweli. Kuanzia sasa nitakuwa nafanya sehemu yangu, na kuukabili ukweli ili niweze kutatua matatizo kabla hayajawa makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 138 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment