Kuna wakati unaweza kuona kama watu wengine wanakunyanyasa au kukushambulia kutokana na hali uliyonayo au kitu unachofanya. Katika hali kama hii unachukua hatua gani? Unalalamika kwa nini watu wakushambulie wewe? Unajiona kama ni mtu mwenye bahati mbaya kutokana na hali ulizo nazo ambazo zinawafanya wengine wakunyanyase na kukushambulia?
Kama hiki ndio unachofikiria au ambacho huwa unafanya, basi unakosea sana. Kwa kufanya hivi unakubali kunyanyasika, unakubali kushambuliwa na hivyo kujiweka katika mazingira magumu zaidi.
SOMA; Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani - 2
Leo nataka nikuambie kwamba hakuna mtu anayeweza kukunyanyasa, hakuna mtu anayeweza kukushambulia kama wewe hutampa ruhusa hiyo. Na ruhusa unayompa sio kwamba unamwambia haya ninyanyase, hapana, ila ni pale unapopokea manyanyaso yake au mashambulizi yake.
Kama unataka kumyima mtu nafasi ya kukunyanyasa au kukushambulia, basi puuza chochote anachosema ili kukunyanyasa au kukushambulia. Kwa kufanya hivi utakuwa umezuia madhara yoyote ya manyanyaso hayo yasije kwako. Ila kama utaanz akuyapa uzito yale ambayo anasema, utaanza kujisikia vibaya, utaanza kujiona wa chini na hatimaye kuruhusu kunyanyasika.
Watu wanaotaka kukunyanyasa au kukushambulia ndio wenye matatizo makubwa kuliko hata ambayo unayo wewe. Hivyo badala ya kulalamika au kupambana nao, waonee huruma, maana wao wenyewe wanapitia manyanyaso makubwa sana.
SOMA; Kila Suluhisho Linatengeneza Tatizo, Chagua Ni Tatizo Gani Unataka.
TAMKO LA LEO;
Najua hakuna mtu yeyote anayeweza kuninyanyasa au kunishambulia bila idhini yangu. Kuanzia sasa nitampuuza mtu yeyote anayesema maneno ya kulenga kuninyanyasa au kunishambulia. Najua mtu huyu ana matatizo makubwa ndani yake na ndio maana anaona raha pekee aliyonayo ni kunyanyasa wengine, sasa mimi hakuna anayeweza kunipata.
Tukutane kwenye ukurasa wa 140 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment