Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, April 6, 2015

UKURASA WA 96; Kila Suluhisho Linatengeneza Tatizo, Chagua Ni Tatizo Gani Unataka.

Tulishakubaliana kwamba hakuna maisha ambayo hayana matatizo. Kila maisha yana changamoto zake na huwezi kuzikimbia changamoto kwenye maisha. Kama unafikiria maisha ambayo hayana changamoto basi hayo ni maisha ya ufu. Yaani maisha yako yatakoma kuwa na changamoto pale ambapo utakufa. Lakini wakati wote ambao utakuwa hai, matatizo na changamoto ni sehemu ya maisha yako.

SOMA; UKURASA WA 75; Kila Mtu Ana Matatizo…

Jambo muhimu unalotakiwa kujua kuhusu matatizo ni kwamba unaweza kuchagua ni matatizo gani ambayo unayataka. Namaanisha kwamba matatizo uliyonayo sasa uliyachagua mwenyewe, iwe ulikuwa unajua au la.

Leo nataka nikushirikishe mbinu muhimu itakayokusaidia kuchagua matatizo ambayo utaweza kuyatatua.

SOMA; Usinunue Matatizo Ya Watu.

Iko hivi, kila tatizo ambalo unalo kwenye maisha yako utakapolitatua utatengeneza tatizo jingine. Yaani suluhisho la tatizo moja linazaa matatizo mengine. Hivyo kabla hujatatua tatizo fikiria ni tatizo gani unalokwenda kutengeneza kwa suluhisho lako hilo.

Kwa mfano kama una hasira na msongo wa mawazo unaweza kuona njia ya kutatua tatizo hilo ni kupunguza mawazo yako. Kuna njia nyingi za kupunguza mawazo, kama utachagua njia ya ulevi, maana yake unatengeneza matatizo makubwa zaidi baadae.

Na mara nyingi suluhisho ambalo ni rahisi linatengeneza tatizo kubwa zaidi baadae.

Chunguza kila suluhisho unalofikiria wkenye matatizo yako na chagua lile ambalo litakuletea matatizo madogo na utakayowez akuyamudu.

SOMA; Njia Mbili Za Kukuondolea Matatizo Yako Ya Kifedha.

TAMKO LA LEO;

Najua kwmaba maisha yangu hayatakoma kuwa na changamoto na matatizo. Nafahamu pia ya kwamba suluhisho lolote la matatizo yangu linatengeneza matatizo mengine. Kuanzia sasa nitachunguza suluhisho lolote ninalotaka kuchukua ili kuhakikisha tatizo litakalotokea naweza kulimudu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 97 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment