Kila mtu huwa anaongea na nafsi yake si ndio? Kila siku na kila mara kabla ya kufanya jambo lolote huwa unaiuliza nafsi yako, je hili ni jambo muhimu la kufanya? Je nitaweza kulifanya vizuri? Je wengine watanionaje nitakapolifanya? Je nikishindwa kulifanikisha itakuwaje?
SOMA; BIASHARA LEO; Umuhimu Wa Hadithi Ya Biashara Yako.
Na hata baada ya kufanya jambo lolote pia huwa unaongea na nafsi yako. Huwa unajiuliza maswali kama, je nimefanikisha kile nilichotaka? Je watu wameona nilivyo muhimu? Je nimeweza au nimeshindwa?
Hii ni sehemu fupi sana ya mazungumzo yako wewe na nafsi yako. Sehemu kubwa ya mazungumzo yako na nafsi yako ni mazungumzo ya kujikosoa. Haya ni mazungumzo ambayo yanakufanya uone huwezi na kukukatisha tamaa.
SOMA; Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo - 2
Mazongumzo ya kujikosoa unayozungumza na nafsi yako ni sumu kubwa sana kwako kufikia mafanikio. Hata kama ungepewa mbinu nzuri kiasi gani za kufikia mafanikio, kama bado utaendelea kujikosoa mwenyewe huwezi kupiga hatua yoyote. Na hii ndio sababu kubwa kwa nini miaka yote unaweka malengo lakini unashindwa kuyafikia, umekuwa ukijikosoa na kujikatisha tamaa hivyo kuogopa hata kujaribu.
Anza mazungumzo mazuri na nafsi yako. Fanya mazungumzo chanya, jipe moyo, penda kujaribu na jipongeze kwa hatua yoyote unayopiga. Pale ambapo mazungumzo ya kujikatisha tamaa yanaanza yaondoe haraka na jipe mazungumzo ya kukuhamasisha kuchukua hatua na kuendele akujaribu hata kama hupati majibu uliyokuwa unategemea.
SOMA; Hiki Ndicho Kitu Pekee Chenye Nguvu Kubwa Ya Kubadilisha Maisha Yako Kabisa.
TAMKO LA LEO;
Najua mazungumzo yangu na nafsi yangu ni muhimu sana na yana ushawishi mkubwa kwangu. Kuanzia leo nitaondoa mazungumzo yote ya kujikatisha tamaa na kuweka mazungumzo ya kunipa moyo na kunihamasisha. Najua kw akuendekeza mazungumzo ya kujikatisha tamaa kutaninyima fursa nyingi za kuweza kufikia mafanikio makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 95 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment