Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, April 24, 2015

UKURASA WA 114; Tumia Vikwazo Ulivyonavyo Kufikia Mafanikio.

Watu wengi huamini kwamba ili uwezekufikia mafanikio basi unahitaji uwe na vitu vingi sana au uweze kufanya vitu vingi. Hii inaweza kuwa kweli ila kuna ukweli unaotakiwa kuujua na unaweza kukushangaza sana.

Ukiwachukua watu wawili, na mmoja akawa ana vitu vingi na kuweza kufanya vitu mbalimbali, mwingine akawa na vitu vichache na kuweza kufanya vichache pia. Kwa nafasi kubwa mwenye vitu vichache anaweza kufanikiwa kuliko mwenye vitu vingi.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Unajua ni kwa nini? Twende pamoja.

Unapokuwa na vitu vichache au unapoweza kufanya vitu vichache, nguvu zako zote unazipeleka kwenye vitu hivyo vichache. Na siku zote unapoweka nguvu zako zote kwenye vitu vichache, hakuna jinsi mafanikio yanaweza kujificha.

Unapokuwa na vitu vingi au kuwez akufanya vitu vingi, unapoteza muda mwingi kwenye vitu hivyo na hatimaye kushindwa kufanikiwa hata kwenye kimoja.

Badala ya kulalamika kwamba umekosa hiki au umekosa kile ndio maana hufanikiwi, hebu tumia vile vichache au kile kimoja ulichonacho kuwez akukufikisha kwenye mafanikio. Unaweza kupika mandazi tu? Hebu jifunze vizuri kuhusu upishi wa maandazi, hebu pika mandazi matamu sana ambayo watu watayafurahia, hebu yatangaze maandazi yako popote unapokuwa na hebu toa mafunzo ya upishi wa maandazi.

SOMA; Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.

Unaweza kulima tu? Hongera. Sasa hebu fuatilia kilimo unachofanya ili ukijue vizuri, hebu jua mbegu bora za kupanda kwa eneo unalofanyia, hebu jua masoko ya mbali zaidi na yenye faida kubwa badala tu ya kukubali kulanguliwa.

Huna miguu? Hebu tumia mikono yako vizuri, kufanya kazi za mikono ambazo zitakuwezesha wewe kufikia mafanikio makubwa.

Unataka kuanza biashara ila huna mtaji? Hapo ndio pazuri pa kuanzia kwa sababu, kwanza huna kitu kingine cha kufanya. Pili huwezi kupata hasara. Sasa ni jukumu lako kujua ile biashara unayotaka kuifanya, kujua kiwango cha chini kabisa unachoweza kuanzia na kuanzakufikiria utawezaje kupata kiwango hiko cha chini

Huna elimu? Safi sana, sio safi kwa sababu huna ila safi kwa sababu hutakuwa na sababu. Pale utakapoamua kuingia kwenye shughuli yoyote hutaanza kufikiria mimi na elimu yangu nafanya hivi! Wewe utachakarika kwa sababu unajua huna tumaini jingine, na utawaacha wenye elimu zao wakishangaa wakati wewe unafanikiwa.

SOMA; Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.

Kikwazo chochote ulichonacho kwenye maisha yako, usikilalamikie, bali kitumie kufikia mafanikio.

TAMKO LA LEO;

Vikwazo nilivyonavyo ni fursa kubwa sana kwangu kufikia mafanikio makubwa. Vinaniwezesha kuweka nguvu zangu kwenye mambo machache ninayoweza kufanya na kwa njia hii mafanikio ni lazima kwangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 115 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment